Watu wengine hujiuliza ndege hutumia mafuta gani?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Aviation Fuel ni mafuta yanayotumiwa kuendeshea injini za ndege. Kimsingi zipo kama aina nne za mafuta zinazotumika katika usafiri wa anga.
  • Jet A-1, ambayo kimsingi ni kundi la mafuta ya taa.
  • Jet B, ni mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli.
  • Avgas, ambayo ni kama petrol ya ndege.
  • Biokerosene ambayo ni mchanganyiko wa mafuta ya taa na mafuta mimea.

JetA-1
Mafuta haya pia huitwa JP-1A hutumiwa ulimwenguni kote katika injini za turbine (injini zenye mfumo wa 'jet na turboprops')

Haya ni kama mafuta ya taa yaliyosafishwa kwa uangalifu ambayo yapo fanisi kuwaka kwenye joto la kiwango cha 38 °C na kiwango cha chini -47 °C.

Mafuta haya ya taa yanasafishwa kwa ustadi mkubwa sana na baada ya kusafishwa yanachanganywa na kiwango kadhaa cha viambatanishi vinavyo wezesha kuwaka katika hali iliyodhibitiwa, kuzuia viumbe kukua ndani yake kama fangasi, bakteria, pia kuzuia kuganda kwenye ubaridi wa -30°C n.k

Ndege za kijeshi mfano za NATO hutumia mafuta haya na viongezeo maalum zaidi na kuitwa jina la Jet-Propellant-8 (JP-8).

Jet B
Mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli. Mafuta haya hutumiwa sana katika ndege za kijeshi.

Mchanganyiko huu maalum wa daraja la Jet B, pia huitwa JP-4 ambapo Petroli asilimia 65% na Mafuta ya Taa asilimia 35%.

Haya hutumiwa zaidi kwenye sehemu zenye ubaridi sana kwa sababu yanaweza kuwaka kwa joto la 20°C.
Lakini pia injini lazima ziwe zimeundwa maalum kwa matumizi ya mafuta haya.

AvGas (Aviation Gasoline)
Hii ni kama Petroli maalum kwaajili ya ndege hasa zile zenye injini za piston.

Mafuta haya katika usafiri wa anga kawaida hutumiwa tu katika injini za zamani za Piston hasa ndege za michezo, ndege ndogo za kibinafsi ambazo zinahitaji mafuta ya kuongezwa kiasi kikubwa cha octane.

Kwahiyo Avgas ni kama petroli iliyoongezwa octane 100 ili kukidhi mahitaji haya.

Hapa Ulimwenguni ni aina ya Avgas100LL tu ambayo bado inapatikana kirahisi na ndege zilizo na injini ya petroli tu ndiyo zinaweza kuendeshwa na avgas, ndege zinazotumia turbine au zile zilizo na injini za mfumo wa kerosene/dizeli zinahitaji jetA.

Kwa kuwa avgas ni ghali, kuna mabadiliko ya kuongezeka kwa mafuta ya dizeli na mafuta ya taa.
Bei kubwa hutokana na kiwango cha chini cha uzalishaji, njia ndefu za usambazaji, na ufafanuzi wa udhibiti wa ubora.

Biokerosene
Biokerosene mchanganyiko wa mafuta ya taa na nishati ya mimea ambayo tasnia ya usafiri wa anga.

Screenshot_20221107_145838.jpg
 
Attachments

  • images (24).jpeg
    images (24).jpeg
    38.1 KB · Views: 30

View attachment 2409321

Meneja wa makampuni, asante kwa kutupatia hii elimu. Mimi sina ndege na wala sitarajii kununua ndege 🤣, kwakuwa wewe ni mtaalamu wa mafuta (liquid fuels expert/enginer) hebu unisaidie kitu; je inawekana kutumia Biofuels specifically ratio fulani ya Biokerosene kupikia katika kerosene stoves ili kupata matokeo chanya??
 
Back
Top Bottom