SI KWELI Watu wenye kundi la damu O+ hawawezi kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI

SI KWELI Watu wenye kundi la damu O+ hawawezi kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwa na uvumi kuwa watu wenye kundi la damu O+ hawawezi kupata maambukizi ya VVU/ UKIMWI. Hata hivyo, wanasayansi wanasema kundi la damu halina uhusiano wowote na kutopata maambukizi ya UKIMWI.


JE NI KWELI UKIWA NA KUNDI “O” LA DAMU HUWEZI PATA MAAMBUKIZI YA UKIMWI?

1657977651137.png
 
Tunachokijua
Madai ya kuwepo wa baadhi ya makundi ya damu yasiyo na uwezo wa kuambukizwa VVU yamekuwepo kwa muda mrefu. Mara nyingi, Kundi O ndilo huhusishwa na madai haya.

JamiiForums imebaini kuwa kila kundi la damu lina hatari sawa kupata maambukizi ya VVU endapo utajiingiza kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kupata VVU, kuwa na aina yoyote ya kundi la damu siyo kigezo cha mtu kutoambukizwa virusi vya UKIMWI endapo usipozingatia tahadhari mfano; kufanya mapenzi bila kinga, kuchangia au kupokea damu isiyopimwa na wataalamu wa afya, na kuchangia vitu venye ncha kali na mtu mwenye maambukizi.

Uwezo wa kuambukizwa VVU kwa mtu yeyote mwenye aina mbalimbali za damu hata kwa mwenye kundi O la damu ni mkubwa, virusi huingia mwilini mwako kutokana na kuchanganyika kwa damu mtu mwenye VVU. Inapokuwa ndani ya mwili wako, inashambulia Seli zako za Msaada za T3 ambazo ni sehemu ya mfumo wako wa kinga.

JamiiForums inathibitisha kuwa Wazo kwamba aina ya kundi O inatoa ulinzi ni hadithi potofu. Wanasayansi wamebaini kwamba baadhi ya watu wanaweza kuwa sugu kwa virusi hivyo kijeni, lakini hii haihusiani na aina za damu za ABO.

VVU haijali kundi lako la damu, wala virusi vingine. kundi la damu karibu kamwe havihusiani na chochote isipokuwa ujauzito, hazikupi kinga dhidi ya magonjwa, VVU huambukiza aina zote za damu ikiwa ni pamoja na kundi la damu O.

Aina za damu huamuliwa na antijeni kwenye uso wa seli nyekundu za damu, na seli nyekundu hazina jukumu lolote katika kuwezesha maambukizi ya VVU kwa njia yoyote. Kwasababu virusi vya UKIMWI (VVU) huambukiza seli nyeupe za damu, ambazo hazina jukumu lolote katika kuamua aina za damu.

VVU hushambulia aina maalum ya seli za mfumo wa kinga mwilini, zijulikanazo kama Seli Msaidizi wa CD4 au Seli T. Wakati VVU inapoharibu seli hii, inakuwa vigumu kwa mwili kupigana na maambukizi mengine.
Back
Top Bottom