Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
We! Wakati Tanganyika inapata uhuru maisha yalikuwa safi sana, hakukua na wizi, miji ilikuwa misafi, hospitali zilimtibu kila mtu na chakula kwa wagonjwa kilikuwepo, shule zilikuwa safi na mwanafunzi alipata elimu bora yenye kiwango cha ulaya na alipewa kila kitu shuleni kasoro unifomu.hao wajingawajinga wa south africa wengi wahajatoka kutembelea nchi nyingine za Afrika ili waone uhalisia wa MIJITU MYEUSI.
📌📌Yule kichaa MALEMA angewapa tour waje hata hapa EAC wajionee maajabu ya nchi zenye kujisifu kupata uhuru miaka zaidi ya 60 ila ni kama zimepata uhuru mwaka jana😀😀😀
Nimalizie kwa kukujulisha kuwa thamani ya fedha ilikuwa sawa na ya Uingereza, tatizo tulipopata uhuru viongozi wakaanza kugawana alivyoviacha mwingereza na kuanza kutudanganya eti idadi ya wananchi ni kubwa! Yaani ghafla?