Watu zaidi ya 50 wauawa Uganda

Watu zaidi ya 50 wauawa Uganda

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,496
WATU ZAIDI YA 50 WAUAWA UGANDA

Watu wasiopungua 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi na kambi za jeshi nchini Uganda, kwa mujibu wa jeshi.

Miongoni mwa waliokufa ni washambuliaji 41 na polisi pamoja na raia 17.

Mashambulio hayo yametokea magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Jeshi limesema mashambulio hayo yalisababishwa na mzozo baina ya makabila hasimu, lakini kuna wasiwasi wa uwezekano wa kuzuka kwa waasi wa Uganda waliopo Mashariki mwa Kongo.

Mashambulio hayo yamelenga majeshi katika wilaya za Kasese, Ntoroko na Bundibugyo.

Msemaji wa jeshi amesema mashambulio hayo hayana uhusiano wowote na kundi la waasi la ADF, ambalo lilikuwa likifanya shughuli zake katika eneo hilo zaidi ya muongo mmoja uliopita.

"Tunachofahamu ni kuwa wanamgambo hawa hawana uhusiano na ADF-NALU, lakini tunachunguza kuona sababu hasa na nani wanawaunga mkono," amesema Paddy Ankunda, msemaji wa jeshi akizungumza na shirika la habari la Reuters.

Watu 17 walikamatwa na wanahojiwa kwa mujibu wa polisi.

Source: Salim Kikeke facebook page - BBC
 
Duh.God bless Tanzania, tuepusha na haya..yakktokea haya ntakuwa mgen wa nan mm!!! Ntakmblia wap nkapona na maafa haya...
Pole ziwafikie jiran zetu Uganda.Mungu awape ulinzi, ndcho nachoweza kusema.
So sad yaan
 
Zame ya mseveni kuomboleza baada ya kenyatha kupoa kidogo.
 
Nusura Nimeseme Ni Al shabab Wakati Huu Kwao Ni Mwezi Mtukufu,Maana Hata Boko haram Wamekataa Kuachia Wale Wasichana !
 
Last edited by a moderator:
Zame ya mseveni kuomboleza baada ya kenyatha kupoa kidogo.

kichaa utajua kwa maneno yake gaidi mkubwa badala ya kuwapa pole unaandika ujinga wako ...poleni sana wafiwa wote tunamwomba Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Ni LRA hao, payukeni ukweli.

Mnaogopa kuwaita Wakristo wenzenu ma terrorist?
 
Ni LRA hao, payukeni ukweli.

Mnaogopa kuwaita Wakristo wenzenu ma terrorist?

Hoja si ukristo..hoja ni je unaunga mkono Matendo yao???...haijalishi mwenye dini gani katenda...even if it were LRA..their evils are not to be justified ...they should be strongly condemned. .just like any other extremist organisation. ..
 
Ni LRA hao, payukeni ukweli.

Mnaogopa kuwaita Wakristo wenzenu ma terrorist?

Yaani ukristo ni mzigo mzito,wanashindwa kukumbuka kwamba marekani imesitisha misaada nchini UG kwa kukataa ushoga.
na moja ya misaada hio ni ulinzi.sasa usishangae hilo kundi linadhaminiwa na marekani kwa mlango wa nyuma.

"wala hawatakuwa radhi mayahudi wala manaswara mpaka mnatakapo fuata mila yao"
 
Hoja si ukristo..hoja ni je unaunga mkono Matendo yao???...haijalishi mwenye dini gani katenda...even if it were LRA..their evils are not to be justified ...they should be strongly condemned. .just like any other extremist organisation. ..

Huwezi kusikia wakisema magaidi wa kikristo
 
na babu ndio anajiandaa kuingia madarakani kwa mara ingine tena aaah kuna nchi ngumu jamani nashukuru kuzaliwa tanzania
 
Hoja si ukristo..hoja ni je unaunga mkono Matendo yao???...haijalishi mwenye dini gani katenda...even if it were LRA..their evils are not to be justified ...they should be strongly condemned. .just like any other extremist organisation. ..

Mbona hamshutumu?
 
Back
Top Bottom