Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa na historia ya nchi yetu kwa muda mrefu sasa katika vyombo mbali mbali vya hbr. Nimegundua mambo kadhaa kutoka kwa waandishi na wadau wake. Wengi baadhi ya waandishi na baadhi ya wadau wa habari wamekuwa wakichambua mambo ya siasa na utawala wa nchi yetu kwa kutosimamia ukweli na uhalisia. Wengi hugemea au kupendelea upande wa dini au kabila waliko wao. Hata kama upande huo una haribu nchi wao hujifanya hawaoni. Kwa hiyo hata humu JF kuna watu sasa hivi wanaiponda au kutoiunga mkono serikali iliopo madarakani jwa sababu sio watu wa imani moja au kabila moja. Na pia kuna wengine wanaiunga mkono sio kwamba inafanya vizuri bali ni kwa kuwa tu ni wamoja ktk dini au kabila. Tukitaka kwenda mbele kama nchi tubadilike tuache unafiki. Nyeusi tuseme nyeusi na nyeupe isemwe tu kuwa nyeupe bila kuogopa wala kupendelea.