Watuhumiwa 10 wa uhalifu wakamatwa Kibaha Pwani

Watuhumiwa 10 wa uhalifu wakamatwa Kibaha Pwani

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jeshi la Polisi Tanzania lipo kwa mujibu wa sheria mama yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 147. Moja ya majukumu yake kwa mujibu wa sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322 kifungu cha 5 (1) ni Kulinda maisha ya watu na mali zao pamoja na Kubaini na kuzuia uhalifu.

Katika kutekeleza jukumu la kubaini na kuzuia uhalifu, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani tarehe 16/08/2025 lilipata taarifa za uwepo wa watu katika Ukumbi wa Mwitongo huko Mailimoja Shule, Wilaya ya Kibaha, wanapanga njama za kufanya uhalifu.

 
Back
Top Bottom