PostGE2025 Watuhumiwa 20 wa uhaini waachiwa huru, Niffer kuendelea kusota rumande

PostGE2025 Watuhumiwa 20 wa uhaini waachiwa huru, Niffer kuendelea kusota rumande

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Watuhumiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini wameachiwa huru leo Novemba 25, 2025.

Shauri lililokuwa linawakabili watuhumiwa hao leo lilikuwa linaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Aaron Lyamuya, ambapo wakili wa Serikali Mkuu Titus Aaron alieleza mahakama kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Mkuu (DPP) amesema hana nia ya kuendelea na mashauri ya washtakiwa 20.

Katika shauri hilo walikuwa washtakiwa 22 na wanaorudishwa gerezani ni Jenifer Jovin(Niffer) na Mika Lucas Chavala.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Novemba 7, 2025.

1764085821992.png
 
Naye atatoka tu ,wamemuweka ili dau la kutoka liwe REFU ,ndugu pasukeni kibunda ili atoke haraka.
 
Wanapoteza muda tu, yaani huyo dada na huyo mwenzake wanaweza kuwa wahaini??Tunaupumbavu na ujinga mwingi sana.Nahisi watawala wana - hamu na uhaini, ngoja siku watokee wahaini orginal, ndo tutaelewa tofauti ya Niffer na mhaini.
Mtu muuza vipodozi hapo sinza, mtu wa mitandaoni...anakua mhaini???
 
Back
Top Bottom