mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema tayari vyombo vya dola vimeshawatia nguvuni watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa msichana anayedaiwa kuwa ni mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.
Agosti 4, 2024 zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu.
Kadhalika, katika video hiyo inayodaiwa kuchukuliwa na vijana hao, binti huyo alisikika akieleza anakotokea na kumwomba msamaha mtu aliyetambulishwa kwa jina la afande.
Masauni amethibitisha kutiwa nguvuni kwa vijana hao leo, Jumanne Agosti 6, 2024 alipotafutwa na Mwananchi Digital kwa njia ya WhatsApp.
Katika ujumbe mfupi aliotumiwa kuulizwa iwapo watuhumiwa hao wameshakamatwa, Masauni alijibu kwa kuandika “tayari” kupitia ujumbe huohuo wa njia ya WhatsApp.
Hata hivyo, Waziri Masauni hajafafanua zaidi kwani amesema bado yupo kwenye mkutano kwa sasa.
Pia soma

- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu
- Suala la binti aliyefanyiwa ukatili wa kulawitiwa, tunahitaji kauli ya Rais ili Polisi watende haki na Mahakama ifanyekazi yake
- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa mande na wanaume watatu
- Peter Madeleka: Ikiwa DPP Mwakitalu hatawapeleka mahakamani ndani ya saa 24 waliombaka binti wa Yombo, mimi nitawapeleka
- TLS yalitaka Jeshi la Polisi kuwatia nguvuni waliohusika na kitendo cha udhalilishaji na ukatili wa kijinsia kilichotokea Yombo Dovya
- News Alert: - Watu 4 wanaotuhumiwa kutumwa na 'afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya Mkoani Dar, Wafikishwa Mahakamani