Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Makosa ya ubakaji na ulawiti yapo mbioni kuondolewa dhamana kutokana na Serikali kuanza mchakato wa kufanyia marekebisho Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Hatua hiyo imetokana na utafiti mdogo uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuonesha kuwa baadhi ya watuhumiwa wa makosa hayo wakiwa nje kwa dhamana wanakimbia na wengine kuharibu ushahidi au kumalizana na wazazi ama ndugu wa muathirika wa vitendo hivyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Happy Msimbe, aliyasema hayo jana kwenye kikao kilichowakutanisha wataalam na wadau wa masuala ya sheria kutoka Wizara, Taasisi za serikali ili kutoa mapendekezo ya sheria hiyo.
Alisema nia ya kukutana na wataalam hao ni kupata maoni yatayosaidia kujenga hoja ya kufanya makosa hayo kutokuwa na dhamana ili kupunguza matukio hayo kwa jamii.
Mkurugenzi huyo alisema wanalenga kulinda kundi la watoto na wanawake ambao ni waathirika wa vitendo vya ukatili.
“Kikao hiki kimelenga kuangalia na kupitia sheria nyingine ambazo zinamgusa mtoto ili ziweze kuendana na hali halisi iliyopo katika jamii ili kuwasaidia watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili katika jamii,” alisema
Chanzo: Nipashe