Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Washitakiwa wawili wanaotuhumiwa kukutwa na vipande tisa vya meno ya ndovu yenye thamani ya dola za Marekani 30,000, wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iwapangie Gereza la Keko kwa kuwa ni pazuri na pana usafi.
Washtakiwa hao ni Hassan Sangari (22), mkazi wa Kingula mkoani Dodoma na Nassoro Mbuguni, mkazi wa Kibasila, Pwani ambao pia wameiomba mahakama wapewe vitu vyao vilivyopotea katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Dares Salaam.
Sangari na Mbuguni walidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wa mahakama hiyo baada ya kusomewa shtaka moja la kukutwa na nyara za serikali na Wakili wa Serikali Faraja Ngukah.
Baada ya Ngukah kumaliza kuwasomea shtaka lao, washtakiwa walinyoosha vidole na kumwomba Hakimu Shaidi kuwapangia mahabusu ya Gereza la Keko kwa kuwa ni pazuri na pana usafi wa hall ya juu, pia wameshapata marafiki ambao wanawasaidia sabuni na vitu vingine.
Chanzo: Nipashe