Watuhumiwa wawili wanaodaiwa kushirikiana na Sabaya mbaroni

Watuhumiwa wawili wanaodaiwa kushirikiana na Sabaya mbaroni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watu wawili wanaodaiwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo makosa yajinai wanashikiliwa na polisi mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Kilimanjaro, Arterio Kawonga alisema uchunguzi wa matukio yaliyofanywa na Sabaya mkoani humo unaendelea na unafanywa na timu kutoka makao makuu ya ofisi hizo.

Juni 4, mwaka huu Sabaya alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na wenzake watano kusomewa mashtaka sita, likiwamo la uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kupokea rushwa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 18 na kusomewa mashtaka mawili yeye na wenzake wawili ambayo upelelezi wake ulikuwa umekamilika.

“Uchunguzi wa matukio aliyoyafanya Sabaya Kilimanjaro bado unaendelea, utakapokamilika tutawapa taarifa maana bado suala hili lipo mkononi mwa timu yetu kutoka makao makuu, bado wanaendelea na uchunguzi na taarifa ambazo zimepokewa zinaendelea kufanyiwa kazi,” alisema Kawonga.

“Kuna kesi nyingine za kijinai ambazo zipo polisi na tayari kuna watuhumiwa wawili tuliwakabidhi polisi Mkoa wa Kilimanjaro, wengine ni walewale anaoshtakiwa nao Arusha aliofanya nao matukio katika wilaya za Hai na Moshi.”

Juni 15,mwaka huu Kamanda wa Takukuru mkoani humo, Frida Wikesi alisema wanaendelea kuchunguza tuhuma nyingine saba zinazomkabili Sabaya alizozifanya wakati akiwa mkuu wa wilaya.

Wikesi alisema wapo watu wanatajwa kushirikiana na Sabaya kufanya uhalifu na endapo uchunguzi ukithibitisha walihusika, watafikishwa mahakamani.

Pia, alisema wote wanaotajwa kushirikiana na Sabaya kufanya uhalifu katika mkoa huo chunguzi dhidi yao zinaendelea ili waliotendewa uhalifu huo, haki zao zipatikane.

Juni 18, katika Mahakama hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka na wenzake, Abdallah Chagula na Tarsila Garvas, walisoma mashtaka hayo mbele Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu Salome Mshasha huku watuhumiwa wakiwa wanatetewa na Wakili Moses Mahuna.

Kweka alisema upelelezi katika makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha yaliyokuwa yanawakabili Sabaya na walinzi wake wawili upelelezi umekamilika na wapo tayari kuwasomea maelezo.

Akisoma maelezo hayo, Gervas alisema Februari 9, mwaka huu, Sabaya na watuhumiwa wawili Silvester Nyengu na Daniel Mbura, walivamia duka la Mohamed Saad lililopo Mtaa wa Bondeni.

Alisema katika mashtaka hayo ya unyang’anyi walitumia silaha ambayo ni kinyume cha kifungu cha 287(a) cha mwenendo wa makosa ya jinai, kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, watuhumiwa hao baada ya kuvamia duka hilo, waliwalaza sakafuni, kuwapiga na kuwatishia kwa bunduki, Bakari Msangi ambaye ni diwani wa Sombetini (CCM) na Ramadhani Khatibu.

Gervas alisema watuhumiwa hao waliiba Sh390,000 fedha za Msangi, baada ya kumtishia kwa bastola na kabla ya kumpora, Silvester alimfunga pingu Msangi.

Katika kosa la pili watuhumiwa hao walimtishia kwa bunduki Khatibu na kumpora Sh35,000 na simu aina ya Tecno.

Baada ya kusomewa mashtaka, waliyakana na Hakimu Salome aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 2, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa.

Hata hivyo, Wakili Mahuna aliomba upande wa mashtaka kumkabidhi hati ya mashtaka katika shauri hilo na maelezo ya walalamikaji.

Mwananchi
 
FB_IMG_1621624215434.jpg
 
Sabaya aliletwa hai kwa kazi moja tu ya kumshughulikia Mbowe mpaka akose ubunge
 
Juzi nilipita Kkoo kununua mifuko ya Nguo ya ofisini, nikawa napiga stori kidogo na muuzaji yule namuuliza kama bado wanataabishwa na upatikanaji wa mifuko akanambia sasa hivi kuko shwari kabisa, tukazungumza kidogo hapo akanigusia ishu moja ya huyu jamaa.

Ananiambia, kuna siku Mbowe anatoka kwake Moshi anaelekea Dodoma, vikao vilikuwa vinakaribia kuanza, akapata hitilafu kwenye gari lake, akapiga simu nyumbani wamletee gari lingine ili aendelee na safari na ile lipelekwe gereji, dereva wake akafanya vile sasa ile gari ilivyofika gereji, mara wakapata ugeni usiokuwa na taarifa. Sabaya na genge lake wakawa wameingia pale ndani, wakamuulizia fundi mkuu akajitokeza, wakamuomba funguo jamaa akawaambia huo sio utaratibu wa ofisi, kutoa funguo za mteja kwa asiyehusika.

Jamaa akawaamuru vijana wake waanze kuwashughulikia wale mafundi, wale wajomba walikula kichapo mpaka funguo ikaletwa, Sabaya akachukua chumvi wakaitia kwenye injini halafu wakawafungia wale mafundi chooni.

Akaja jamaa yake na huyu bwana alionisimulia mimi, alikuja kupata huduma pale gereji, akakuta mlango upo wazi na hakuonekani mtu. Jamaa akaanza kutafuta, ila panaonekana kama kulikuwa na watu muda mfupi tu uliopita ila sasa hiv pako kimya. Jamaa kuanza kuita, kuita akasikia sauti kwa mbaliii, akaenda stoo, wapi, ndio akasikia mlango unagongwa kwa ndani, kufungua akawakuta mafundi wamefungwa kamba mikono wamefungiwa chooni ndio kuwafungulia wakamsimulia kilichotokea.

Fundi mkuu akaenda kuripoti polisi, jamaa akaitwa kwa mkuu wa kituo, ile mkuu wa kituo anamuhoji akala makofi nae, Sabaya akasepa. Mkuu wa kituo akapanda ngazi kwa bosi wake akamuelezea kilichotokea bosi akamsihi tu mkuu wa kituo aachane na hilo jambo kwani Sabaya analindwa mzee faza na hawezi fanywa chochote sana mkuu wa kituo anaweza fukuzwa kazi au kupunguzwa cheo.
 
Huyu 7baya alikuwa ni wa kupeleka pale kijazi flyover mnamlaza chali barabarani halafu mnamgonga na semi yenye tani 35
 
Back
Top Bottom