Watuhumiwa wizi wa mil. 700 kwa mramba watoweka

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
_MG_4099.jpg
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova.
Na Makongoro Oging'
WIKI iliyopita katika safu hii tuliandika habari kuhusiana na wizi wa shilingi milioni 700 zilizoibwa kwa Mary Mramba nyumbani kwake Stakishari, wilayani Ilala na tukaahidi kuendelea kuchimbua kilichojiri.
Kufuatia wizi huo wa fedha hizo, habari zinasema kwamba baadhi ya watuhumiwa wametoweka jijini Dar es Salaam na kwa hivi sasa inasemekana wameenda mikoani ambako wamejificha kwa lengo la kukwepa vyombo vya dola.
Vyanzo vya safu ya Fumuafumua ndani jeshi la polisi vinasema kuwa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Ilala linawasiliana na askari ambao wapo mikoa ambayo inadaiwa watuhumiwa wamejificha.
Baadhi ya wapelelezi walikataa kutaja mikoa inayodaiwa wamekimbilia watuhumiwa wa sakata hili.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa wanaotafutwa wametajwa majina yao ambayo ni pamoja na Irine John Bosco Hussen na Dismas Kirya ambao mpaka sasa hawajapatikana.
Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kuwa watuhumiwa waliopo Dar wamekuwa wakiripoti katika Kituo cha Polisi Stakishari ni pamoja na Digna Epimarck Blass na mumewe aitwaye Francis Mushi ambao hata jana Jumatatu walitakiwa kuripoti kituoni hapo.
Mwandishi wetu aliwatafuta watuhumiwa nao bila mafanikio lakini alibahatika kupata namba ya baba wa Digna.
Baba huyo alipopigiwa simu ili azungumzie suala hilo hasa kwa kuwa mwanaye amehojiwa na polisi alisema kwamba sakata hilo lipo polisi hivyo hayupo tayari kulizungumzia.
Mwandishi wa safu hii aliwatafuta Mary na mumewe Boneventura nyumbani kwao Stakishari lakini hawakupatikana na majirani zao walisema kuwa inawezekana wemesafiri, hata hivyo, hakuna aliyejua mkoa au mji waliokwenda .
Fumuafumua ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Komba na alipoulizwa kuhusiana na wizi wa fedha hizo alisema kuwa suala hilo analifuatilia.
“Nina taarifa Mramba alifungua kesi ya kuibiwa fedha hizo nyumbani kwake Septemba mwaka huu na tayari baadhi ya vitu vilivyonunuliwa na sehemu ya fedha hizo vimepatikana,” alisema Kamanda Komba.
 
Ya kaisari mpe kaisari na ya Mramba mwachie Mary! Wacha watekeleze MKUKUTA kwa vitendo!
 
Habari hii nimeipenda hata wangeweza kumwibia akaunti yake yote ingekuwa vema sana! Kodi yetu wanainchi hizo!
 
Mi nimefurah kweli, kwani kuna ubaya gani mwizi akiibiwa alichoiba? mi nawapa big up hao walio ''timba'' hayo ''mafwedha''
 
mmmmmmKWA TWASILA HIYO INONYESHA VIPI WA BONGO WAHASILA YA MAISHA BORA KWAKILA MAZAWA Haya na wao waseke vibaya nao pia zitasogezwa tena
 
_MG_4099.jpg
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar, Suleiman Kova.
Na Makongoro Oging'
WIKI iliyopita katika safu hii tuliandika habari kuhusiana na wizi wa shilingi milioni 700 zilizoibwa kwa Mary Mramba nyumbani kwake Stakishari, wilayani Ilala na tukaahidi kuendelea kuchimbua kilichojiri.
Kufuatia wizi huo wa fedha hizo, habari zinasema kwamba baadhi ya watuhumiwa wametoweka jijini Dar es Salaam na kwa hivi sasa inasemekana wameenda mikoani ambako wamejificha kwa lengo la kukwepa vyombo vya dola.
Vyanzo vya safu ya Fumuafumua ndani jeshi la polisi vinasema kuwa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Ilala linawasiliana na askari ambao wapo mikoa ambayo inadaiwa watuhumiwa wamejificha.
Baadhi ya wapelelezi walikataa kutaja mikoa inayodaiwa wamekimbilia watuhumiwa wa sakata hili.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa wanaotafutwa wametajwa majina yao ambayo ni pamoja na Irine John Bosco Hussen na Dismas Kirya ambao mpaka sasa hawajapatikana.
Uchunguzi wa Fumuafumua umebaini kuwa watuhumiwa waliopo Dar wamekuwa wakiripoti katika Kituo cha Polisi Stakishari ni pamoja na Digna Epimarck Blass na mumewe aitwaye Francis Mushi ambao hata jana Jumatatu walitakiwa kuripoti kituoni hapo.
Mwandishi wetu aliwatafuta watuhumiwa nao bila mafanikio lakini alibahatika kupata namba ya baba wa Digna.
Baba huyo alipopigiwa simu ili azungumzie suala hilo hasa kwa kuwa mwanaye amehojiwa na polisi alisema kwamba sakata hilo lipo polisi hivyo hayupo tayari kulizungumzia.
Mwandishi wa safu hii aliwatafuta Mary na mumewe Boneventura nyumbani kwao Stakishari lakini hawakupatikana na majirani zao walisema kuwa inawezekana wemesafiri, hata hivyo, hakuna aliyejua mkoa au mji waliokwenda .
Fumuafumua ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Komba na alipoulizwa kuhusiana na wizi wa fedha hizo alisema kuwa suala hilo analifuatilia.
“Nina taarifa Mramba alifungua kesi ya kuibiwa fedha hizo nyumbani kwake Septemba mwaka huu na tayari baadhi ya vitu vilivyonunuliwa na sehemu ya fedha hizo vimepatikana,” alisema Kamanda Komba.

It's a crime to have a lot of money in the house.only in Tanzania
 
Back
Top Bottom