Waswahili walisema ndo ndo ndo si chururuu. Wala Lila na Fila havikupata kutengamana.
Hii ikiwa ni kwa maana halisi ya kuwa awamu ya sita si awamu ile ambayo mahabusu walikuwa wakipigiwa mahesabu kuwa chanzo cha nguvu kazi. Eti kuwa asiyefanya kazi na asile.
- DPP amewafutia kesi waliodaiwa kusafirisha wenye ulemavu, kuwatumikisha
Awamu ile ilitambua rasmi magereza kama chanzo muhimu cha nguvu kazi na mahakama kama chanzo kizuri cha mapato. Bila aibu ikapendekezwa hata mawakili watetezi wa watuhumiwa wawe nao wanaunganishwa vifungoni.
Nani alikuwa na uwezo wa kuyakemea yote haya yaliyokuwa yamepinda? Si bunge, si mahakama, si viongozi wa dini, si iliyojiita kamati ya amani ya dini, nk. Wote waliufyata!
Kwani nini vimezima mihemko ya legacy na kwamba kuifuatilia sasa hakupo tena? Kwani nini vimezima miito ya kuwa na waliokwenda days? Ikobwapi miito ya kuwa na baba wa pili wa taifa? Akili zinarejea. Kumbe kulikuwa na kupigwa upofu?!
Hongera mama Samia jitihada zako za kuikarabati hii nchi zimeonekana na zisiishie kuwa ni utashi wako binafsi. Isije ikawa hatari iko pale pale kuwa ukaja kutoka tukarejea tena Misri.
Mheshimiwa kumbuka ya Mungu mengi. Pamoja na wengi kukuombea ya heri ni nani aijuae kesho? Waswahili waliosema linalowezekana leo lisingoje kesho hakukosea.
Utayari wako kuijenga misingi imara ya nchi hii kuwa yenye haki siku zote bila kujali aliyeko madarakani, kutakuongoza kuliko kuwa na Mama halisi wa Taifa hili atakayekumbukwa daima.
Kwako Mama Samia rais wetu wa JMT ikikupendeza tafadhali, kazi inapoendelea.