Watumiaji wa alkasusu wameongezeka sana

Watumiaji wa alkasusu wameongezeka sana

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,325
Reaction score
7,807
Hichi kinywaji kadili siku zinavyozidi kwenda kinazidi kupata umaarufu mkubwa hasa kwa vijana mida ya jioni wengi wameachana na kahawa wamehamia huku kwenye alkasusu

Ukisikiliza story za vijiweni vijana wanakuambia kinywaji hichi kinasaidia kudumisha ufanyaji wa tendo la ndoa kwa muda mrefu

Tunakumbuka pia dawa ya kupaka vumbi la mkongo ilikuwa inasifa kama hizo lakini mwisho ilikuja kufungiwa na mwenyekiti wa tiba asili na mbadala huku sababu za kufungiwa ni baada yakufanyiwa vipimo dawa hiyo nakugundulika imekuwa inachanganywa na dawa ya viagra au erecto

Nchi zilizoendelea ni ngumu kuingiza kila kitu hasa katika madawa ya binadamu ni vyema ufanyike uchunguzi katika kinywaji hicho ili kubaini kama ni salama kwa watumiaji
 
Back
Top Bottom