robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Picha: Pinterest
Mimi nimeanza kutumia X kwa sasa toka 2017. Niliheshimu mtando huu sana kwa habari nzuri na kwa ufupi kutokwa kwa watu mbalimbali.
Leo hii unaingia X unakuta ndio watu wanaongoza kwa kusambaza video za ngono pamoja na kudhalilisha watu na mwisho naweza sema Facebook ni mtandao wa watu wastaarabu sana.
Jambo lingine ni tabia ya uchochezi wa taarifa hili ni kwamba watu wanasambaza taarifa za uongo kuchafua taswira ya mtu au watu na hili vijana wengi wa X wanaongozwa na hisia kuliko ukweli wa mambo.
Soma Pia: Netblocks: Mtandao wa X (Twitter) umepigwa pini nchini Tanzania
Pia, niwapongeze wale ambao wameendelea kutumia X katika kusaidiana na kujenga jamii kwa maandiko yao.
Hivyo nauliza huko X ni wanafunzi wa darasa la saba au watu wasomi?