Matakataka yashavamia huko, ni kama JF tu kipindi cha nyuma ilikuwa na watu smart sana na hata wale vilaza walikuwa na mipaka yao, lkn kwa sasa kumechafukwa vibaya.
Ni aina tu ya wajinga waliokosa contents kichwani basi wanaamua kupost kila aina ya mawazo yao wakitafta engagement kwa lazima.
Kwa sasa mtandao wa X ukiingia ukascroll nusu saa hujakutana na picha za uchi/contents za ngono basi shukuru sana.
Kwa Tanzania hii members wenye ushawishi huko X karibia 70% ni hao hao vijana wasio wastaarabu, wenye lugha chafu, uchochezi, wasambazaji maudhui ya hovyo, ngono na ujinga mtupu.
Kwa sasa hakuna tofauti kati ya instagram na X kimaudhui kwa upande wa Bongo, maana kote udaku,umbea wanashare, kinachosaidia kubalance maudhui angalau kuna baadhi ya watu wachache sana waliobase kwenye siasa angalau wanatoa ahueni ya maudhui.
Miaka 5 ijayo x itakuwa porn site/mtandao wa watu kujiuza, mtandao wa hovyo kuliko.
Sio mbaya ndio aina ya raia na akili zao tulio nao nchini, ambao ndio hawa hawa mitaani wanaojifanya kondoo kumbe mafichoni(nyuma ya keyboard) ni majangiri
Imagine kuna nyuzi zinaitwa WATOTO WAMELALA THREAD, huko ni hatari kabisa