Watumiaji wenye matumizi makubwa ya Internet nawaomba kidogo/Heavy Internet users

Watumiaji wenye matumizi makubwa ya Internet nawaomba kidogo/Heavy Internet users

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,001
Reaction score
23,449
Ni katika kuelimishana tu na kushtuana kama ilivyokua kipindi kile wakati nikijiona mjanja kulipia DSTV package na kupata vitu vizuri kumbe kuna wajanja wanakula channel zangu za DSTV kwa kutumia huduma za cable, FTA DISH, nk nk. Baada ya kusanuka nikaingia ulimwengu ule nilijishangaa sana kwa kuchelewa kujua vitu.

Sasa leo nimekuja kuulizia tena katika suala la internet. Wenzangu nyie mnatumia kampuni gani kurahisisha mambo, au mnatumia nini kupata Unlimited Data Flow yenye bei nafuu, na bado mkapata kile mlichokihitaji na huduma bora 24hrs?

Kwa upande wangu mimi nilikua mteja wa TTCL kwa muda sana ila baadaye huduma zao zikawa mbovu na takataka kabisa; nikaachana nao nikaamua kuwa mteja wa kampuni moja hivi ya Liquid Telecom ambayo nipo nayo mwaka wa pili huu; hadi hivi sasa sina tatizo nao ila tu kuna vitu nataka kufahamu zaidi kutoka kwa watumiaji wengine.

TTCL kabla sijawaacha kwenye mataa nilikua natumia kifurishi chao cha

Business Gold 3Mbps126,000.00/=

Kwa hawa marafiki zangu Liquid wananipa tabasamu kila iitwapo leo, na kifurushi changu ni cha speed ile ile 3Mbps kinanitosha sana ambacho kwa hawa wao hawana 3Mbps, wao wameanzia

  • 1mbpd, Dedicated Burst up to 5Mbps @ 75 dollar (hiki ndio kifurushi changu)
Wakaenda kwa speed tofauti to 8Mbps ambayo wao wanacharge 180 dollar. Basi hawa ndio Liquid ambao kwangu mimi sioni shida kutoka kwao zaidi tu ni burudani ila sitaki kujiona nina tabasaamu kumbe kuna wenzangu mpo mmeuchuna mahali mnakula tu vitu kama ilivyokua kwenye TV.

Hapa leo nimekuja nahitaji kujua kama kuna kampuni mnayoifahamu inayoizidi Liquid na wenye bei pungufu yao au kama kuna njia nyingine naweza itumia kupata internet unlimited sio kupimiwa halafu mseme ni unlimited kama walivyo Tigo, Voda na mitandao mingine wanaojitangaza wanatoa unlimited wakati ni limited packages.

Karibuni:

Ni kwa wale Heavy Users tu wa internet jamani na walio in this game not less than 2 years. Naombeni ushauri wenu/ushuhuda na vyovyote mnavyoweza nishauri maisha yakazidi kuwa mazuri na matamu zaidi.

Nawasilisha.
 
Hizo dedicated Mbps sijui 3/5/8 unazitumia katika devices zipi? How many pcs? How many smartphones? Tuanzie hapo kwanza! Maana wengine ni bundle la simu moja. Mwingine hadi smart TV na familia nzima kwa kutumia home broadcast routers! Wengine internet cafe. Wengine kampuni kabisa yenye significant users.

Tunaomba mchanganuo wa matumizi yako kwanza!
 
Kuna Jamaa alisema ZUKU wana internet very cheap...ni FIBER na unapewa na IPTV.. hebu check kwa website yao

Sent using Jamii Forums mobile app
ni kweli zuku wanayo ila kwa Dar wapo k.koo,oysterbay na mtaa flani sikumbuki jina

bado hawajasambaa sehemu nyingi,sasa sisi wengine tuko huku nnje ya miji ila zuku

hata package zao bei ziko chini sana,sijajua tu kuhusu huduma zao.
 
Hizo dedicated Mbps sijui 3/5/8 unazitumia katika devices zipi? How many pcs? How many smartphones? Tuanzie hapo kwanza! Maana wengine ni bundle la simu moja. Mwingine hadi smart TV na familia nzima kwa kutumia home broadcast routers! Wengine internet cafe. Wengine kampuni kabisa yenye significant users.

Tunaomba mchanganuo wa matumizi yako kwanza!
1. device (pc)

matumizi ni mengi ila kwa siku natumia si chini ya 50GB - 100GB ikitokea

nimefungua ofisi nusu siku,ila kwa Full Day nikicheza rough zangu

zote natumia 130gb - 150gb PER DAY.
 
Mi natumia zuku mkuu, 10 mbps 69,000. Ila ipo mijini tu, na siku hizi wana offer uki renew kabla ya tarehe kuisha wana double speed inakuwa 20mbps.

Kama upo pembezoni vifurushi vya usiku ndio best bet tafuta simu nzuri yenye flagship soc hata kama ya zamani kidogo utapata speed nzuri ya 4g. Kwa halotel unaweza download hadi GB 100 kwa usiku mmoja.
 
ni kweli zuku wanayo ila kwa Dar wapo k.koo,oysterbay na mtaa flani sikumbuki jina

bado hawajasambaa sehemu nyingi,sasa sisi wengine tuko huku nnje ya miji ila zuku

hata package zao bei ziko chini sana,sijajua tu kuhusu huduma zao.
ZUKU wapo vizuri SANA...Upanga, baadhi ya maeneo Kinondoni wanapatikana...ni declare nimewahama TTCL niko na Zuku...

Everyday is Saturday....................😎
 
Mi natumia zuku mkuu, 10 mbps 69,000. Ila ipo mijini tu, na siku hizi wana offer uki renew kabla ya tarehe kuisha wana double speed inakuwa 20mbps.

Kama upo pembezoni vifurushi vya usiku ndio best bet tafuta simu nzuri yenye flagship soc hata kama ya zamani kidogo utapata speed nzuri ya 4g. Kwa halotel unaweza download hadi GB 100 kwa usiku mmoja.
Hakika Sikukosea kuku tag hapa,naomba maelekezo zaidi mkuu kuhusu hiyo Halotel chief

Naomba na msaada wa simu gani nzuri chief hata kwa picha NINGEFURAHI SANA ktk hili.

usipite ukaacha sema kitu hapa Chief-Mkwawa
 
1. device (pc)

matumizi ni mengi ila kwa siku natumia si chini ya 50GB - 100GB ikitokea

nimefungua ofisi nusu siku,ila kwa Full Day nikicheza rough zangu

zote natumia 130gb - 150gb PER DAY.
Hapo sawa! Kwa kiwango ulichosema ni kwa level ya multi users na inabidi huwe na ISP (Internet service provider) anayesomeka na ambaye si mbabaishaji! Wengi wa ma_ISP wanakuwa sio wakweli!

Mkataba unasema anakupa dedicate (let say 3mbps) anaanza kumonitor matumizi yako kwa muda wa masaa au siku au wiki au pengine mwezi alafu anachora trend graph ya matumizi yako kiasi kwamba wakati matumizi yako yapo chine hiyo dedicated subscription channel yako anaanza kuishare (shared) anakuibia na kuwauzia wengine!

Tuchukulie kiwango chako cha chini cha 3mbps ni sawa na 3x60 = 180mb per minute na nisawa na 180x60=10.8Gb per hour na nisawa na 259.2Gb per day.

Haya ni matumizi ya mtu anayezalisha sio matumizi ya porojo! All in all jaribu kuwasiliana na COSTECH wanatumia mkongo wa taifa watakupa mwongozo! Bei zao ni competitive Ila ni waswahili kwavile kuna share za serikali
 
Naamini kwa kazini mchana nikitumia hawa liquid,usiku nyumbani hao Halotel

wanaweza kuwa msaada kwa usiku,ila nini kinahitajika Chief-Mkwawa ?
 
Lakini pia napenda kushare nanyi hili wazo, Hivi mnajua hawa TTCL wana internet kwenye zilw nyumba za mawaziri?

Pia gharama wanayotoza huko ni FREE installation na monthly fee yao ni CHEAP.

Niliwahi kwenda pale Makao Makuu pale wakasema ule mradi ni wa kule tu, labda kama hapo baadae uka expand...

Huu mimi ninaona ni upuuzi wa hali ya juu..TTCL wanatakiwa kuwafikia waTanzania wote kwa usawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika Sikukosea kuku tag hapa,naomba maelekezo zaidi mkuu kuhusu hiyo Halotel chief

Naomba na msaada wa simu gani nzuri chief hata kwa picha NINGEFURAHI SANA ktk hili.

usipite ukaacha sema kitu hapa Chief-Mkwawa
mkuu unahitaji flagship angalau kuanzia mwaka 2015 simu kama note 5 ama s6 kupanda, ikiwa s7, s8, s9, s10,s20 ni bora zaidi, na sio lazima iwe ya samsung kampuni yoyote kubwa inayotumia snapdragon soc inafaa, ikiwa oneplus, sony, lg, xiaomi etc cha muhimu iwe na snapdragon highend kama sd 820, 835, 845, 855, 865 etc. ili upate speed kubwa halotel simu yako inabidi iwe na;

1.mimo 2x2 hii ni multiple input na output, uwezo wa simu kupokea mawimbi minara miwili kwa mpigo inaongeza sana speed.
2. band 2600 ya 4g, hii inapatiakana simu chache, michina mingi hawana
3. download speed kubwa na upload kubwa, gigabit lte inapendeza zaidi, kuna simu zina lte lakini lte yake haina nguvu ni 150mbps tu.

hivyo ukikidhi vigezo vya kuwa na simu nzuri kama nilivyosema hapo juu hayo mambo matatu hatakusumbua. unaunga tu kifurushi na ku enjoy.
 
Back
Top Bottom