Ni katika kuelimishana tu na kushtuana kama ilivyokua kipindi kile wakati nikijiona mjanja kulipia DSTV package na kupata vitu vizuri kumbe kuna wajanja wanakula channel zangu za DSTV kwa kutumia huduma za cable, FTA DISH, nk nk. Baada ya kusanuka nikaingia ulimwengu ule nilijishangaa sana kwa kuchelewa kujua vitu.
Sasa leo nimekuja kuulizia tena katika suala la internet. Wenzangu nyie mnatumia kampuni gani kurahisisha mambo, au mnatumia nini kupata
Unlimited Data Flow yenye bei nafuu, na bado mkapata kile mlichokihitaji na huduma bora 24hrs?
Kwa upande wangu mimi nilikua mteja wa TTCL kwa muda sana ila baadaye huduma zao zikawa mbovu na takataka kabisa; nikaachana nao nikaamua kuwa mteja wa kampuni moja hivi ya Liquid Telecom ambayo nipo nayo mwaka wa pili huu; hadi hivi sasa sina tatizo nao ila tu kuna vitu nataka kufahamu zaidi kutoka kwa watumiaji wengine.
TTCL kabla sijawaacha kwenye mataa nilikua natumia kifurishi chao cha
| Business Gold | 3Mbps | 126,000.00/= |
Kwa hawa marafiki zangu Liquid wananipa tabasamu kila iitwapo leo, na kifurushi changu ni cha speed ile ile 3Mbps kinanitosha sana ambacho kwa hawa wao hawana 3Mbps, wao wameanzia
- 1mbpd, Dedicated Burst up to 5Mbps @ 75 dollar (hiki ndio kifurushi changu)
Wakaenda kwa speed tofauti to 8Mbps ambayo wao wanacharge 180 dollar. Basi hawa ndio Liquid ambao kwangu mimi sioni shida kutoka kwao zaidi tu ni burudani ila sitaki kujiona nina tabasaamu kumbe kuna wenzangu mpo mmeuchuna mahali mnakula tu vitu kama ilivyokua kwenye TV.
Hapa leo nimekuja nahitaji kujua kama kuna kampuni mnayoifahamu inayoizidi Liquid na wenye bei pungufu yao au kama kuna njia nyingine naweza itumia kupata internet unlimited sio kupimiwa halafu mseme ni unlimited kama walivyo Tigo, Voda na mitandao mingine wanaojitangaza wanatoa unlimited wakati ni
limited packages.
Karibuni:
Ni kwa wale
Heavy Users tu wa internet jamani na walio in this game not less than 2 years. Naombeni ushauri wenu/ushuhuda na vyovyote mnavyoweza nishauri maisha yakazidi kuwa mazuri na matamu zaidi.
Nawasilisha.