Watumishi 6 waliofukuzwa kazi Halmashauri ya Siha wamwangukia Rais Samia, waomba iundwe tume huru

Watumishi 6 waliofukuzwa kazi Halmashauri ya Siha wamwangukia Rais Samia, waomba iundwe tume huru

waziri2020

Senior Member
Joined
May 31, 2019
Posts
197
Reaction score
468
Watumishi 6 waliofukuzwa kazi katika halmashauri ya Siha mkoani Kilimanjaro wamemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia suala lao na kisha kuunda tume huru kuchunguzwa namna walivyofutwa kazi kwa madai kwamba kuna uonevu mkubwa ulifanyika.

Mbali na kufutwa kazi pia wameiangukia tume huru ya haki za binadamu nchini kuchunguzwa tukio la kukamatwa aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Valerian Juwal na mweka hazina ,Frank Maleto na kisha kuweka katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi Sanya Juu kwa muda wa siku 40 bila kufikishwa mahakamani.

Watumishi hao wamedai kwamba wana imani na uongozi wa Rais Samia Hassan katika kutenda haki na hivyo wanamuomba aingilie kati sakata la wao kufukuzwa kazi huku wakidai kuwa walifukuzwa kutokana na majungu na fitina.

Walidai ya kwamba uongozi wa halmashauri hiyo chini ya aliyekuwa mkurugenzi aliyehamishwa ,Ndaki Mhuli pamoja na mkuu wa wilaya hiyo ,Onesmo Buswelu ulikuwa ukiendesha kazi zake kwa majungu,ubabe na vitisho.

Walidai kwamba walifukuzwa kazi pasipo taratibu na sheria za kuwafuta watumishi wa umma kazi kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na wao kutopewa nafasi ya kujitetea.

"Mambo yalifanyika kwa ubabe tu mkurugenzi aliamuru vikao vikae kisha akaazimia tufukuzwe kazi pasipo kupewa nafasi ya kujitetea" walisema

Watumishi hao walidai kwamba endapo serikali itaamua kuunda tume huru ya kuchunguza sakata lao basi Itabaini ukweli na mambo mbalimbali yaliyojificha katika halmashauri hiyo ikiwemo suala la ukiukwaji mkubwa wa sheria za utumishi wa umma.

"Kabla hawa viongozi wawili serikali haijawahamisha mambo yalikuwa yakipelekwa kibabe kibabe tu mkurugenzi na mkuu wa wilaya wakiamua ndio linalotekelezwa" walisema kwa nyakati tofauti

Hatahivyo, walienda mbali zaidi na kusema kuwa wanaiomba tume huru ya haki za kibinadamu nchini kuchunguza na kufuatilia kitendo cha jeshi la polisi wilayani Siha kuwakamata aliyekuwa mweka hazina wa halmashauri hiyo,Frank Maleto na mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Valerian Juwal na kisha kuwaweka mahabusu kwa muda siku 40 bila kuwafikisha mahakamani.

"Tunaiomba tume huru ya haki za kibinadamu kuchunguza suala hili sheria haisemi umkamate mtu siku 40 mahabusu alafu unamwachia tu bila kumfikisha mahakamani" walisema

Walisisitiza kuwa watumishi hao walikamatwa kufuatia amri iliyotolewa na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo,Buswelu ambapo aliiagiza vyombo viwashikilie na baada ya siku 40 waliwaachia ghafla.

Hatahivyo,taarifa kutoka wilayani humo zinadai kuwa Maleto na Juwala bado wanaripoti mbele ya ofisi za Takukuru Wilayani Siha kwa takribani mwaka wa tatu sasa bila kufikishwa mahakamani.

"Kila wakiripoti Takukuru wanapigwa kalenda huu ni mwaka wa tatu sasa wanatakiwa waripoti Takukuru tunajiuliza uchunguzi gani huu mwaka wa tatu?" Walifafanua

Baadhi ya wananchi wilayani Siha wameeleza ya kwamba serikali inapaswa kuitupia jicho halmashauri hiyo kutokana na baadhi ya viongozi wake kutumia ubabe na vitisho.


Pichani chini ni mkurugenzi aliyekamatwa na jeshi la polisi wilayani Siha kwa maelekezo kutoka juu,Valerian Juwal ambapo aliweka mahabusu kwa muda wa siku 40 na kisha kuachiwa huru bila kufikishwa mahakamani,mpaka sasa Juwal anaripoti Takukuru kwa mwaka wa tatu sasa bila kufikishwa mahakamani.

IMG_20210805_212629_580.JPG
 
Valerian asayumamita Koren? Baada ya kupata ukurugenzi ukajisahau ukaamua kuwa mwizi. Pole sana. Rudi mbulu ugombee ubunge.
 
Hao TAKUKURU baadhi yao wamekosa uadilifu kabisa
TAKUKURU Tanga bora ofisi zingefungwatu. Wamegeuka kuwa upande wa watuhumiwa. Uwepo wao hauna tija.
Kudhihirisha ulaji rushwa wao hata kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Tanga na msaidizi wake walisimamishwa kazi wakituhumiwa kwa kula mlungula.
Sasa hao walioachwa hapo duh......Tanga nishamba la bibi atakaye akavune
 
Back
Top Bottom