A
Anonymous
Guest
Mimi ni mfanyakazi wa kada ya afya katika Halmashauri ya Simanjiro, mkoa wa Manyara. Tangu Januari 2026 hadi sasa tumekuwa tukikumbana na changamoto nyingi, lakini kila tunapojaribu kuzungumza au kuuliza, tunaondolewa kwenye makundi ya mawasiliano (groups) na hata “kuremove” kabisa.
Inafikia hatua tukitoa malalamiko tunaonekana kama wasumbufu, na tunajibiwa tu kwamba tutafute fursa nyingine za kufanya kazi. Hali ni mbaya zaidi hasa kwa watumishi walioko vijijini, ambapo mazingira ya kazi ni magumu sana na yanahitaji msaada wa haraka.
Kutokana na malalamiko kuwa mengi, hadi sasa kundi letu limefungwa (mute), na hatuna tena sehemu ya pamoja ya kuwasilisha shida zetu. Tunaomba sana mamlaka husika zitusikilize, kwani hali hii inatunyima haki ya kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zetu kama watumishi wa afya.