KERO Watumishi ajira mpya Ukerewe (kada ya elimu) hatujalipwa pesa za kujikimu

KERO Watumishi ajira mpya Ukerewe (kada ya elimu) hatujalipwa pesa za kujikimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ahsanteni sana JamiiForums kwa kuendelea kutupatia habari na kutupa nafasi ya kufikisha sauti zetu.

Sisi watumishi wa ajira mpya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, kada ya elimu, hadi sasa hatujapokea fedha za kujikimu. Jambo hili linatupa wasiwasi, hasa ikizingatiwa kwamba wenzetu wa kada ya afya katika halmashauri hiyo tayari wamepatiwa stahiki hizo.

Soma Pia: Ajira Mpya Kada ya Afya hadi leo hatujalipwa pesa zetu za kujikimu Halmashauri ya Wilaya ya Kahama

Tunawaomba viongozi na mamlaka husika kutupatia ufafanuzi kuhusu sababu ya ucheleweshaji huu na kuhakikisha nasi tunalipwa fedha zetu za kujikimu kwa wakati.
 
Back
Top Bottom