Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wafanyakazi kutoka idara tofauti mkoani Geita, wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutenga fedha kwaajili ya vifurushi vya Intaneti, ili kuwawezeaha utumaji wa taarifa na madokezo kwa waajiri wao kwa wakati.
Kutokana na kupanda kwa gharama za maisha nchini na baadhi ya watumishi kuishi mazingira ya vijijini,wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye kununua bando la Intaneti huku vipato vyao vikiwa havikidhi uhitaji wao.
Ombi hilo limetolewa leo ijumaa Mei mosi,2026, na Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Geita, Pauline Tinda, wakati akisoma risala kwa niaba ya Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi (Tucta) katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kimkoa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ludete, Kata ya Ludete, mji mdogo wa Katoro wilayani Geita.
Katika taarifa yake,Tinda amesema mifumo ya utendaji kwa watumishi wa Serikali Pepmis, imekuwa na Changamoto wakati wa ujazaji wa taarifa na madokezo ya kiutendaji huku baadhi ya maeneo hasa ya vijijini,yakikabiliwa na mifumo duni ya intaneti.
"Watumishi huingia gharama kununua bando kwakuwa wanalazimika kuingia kwenye mifumo kila siku ili kujaza taarifa na madokezo mbalimbali. Pia, baadhi ya maeneo kukosa mtandao kunasababisha watumishi kushindwa kuwazilisha taarifa zao kwa wakati."