Watumishi kama hawa ndio wanaopaswa kuzingatiwa katika fursa mbalimbali kama Motisha

Watumishi kama hawa ndio wanaopaswa kuzingatiwa katika fursa mbalimbali kama Motisha

severinembena

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2018
Posts
2,435
Reaction score
2,402
Swalama wakuu?

Hivi watumishi wenye jitihada kama walimu Wa Shule ya Sekondari Kisimiri kama huyu mkuu Wa Shule Na Mwalimu Wake wa taaluma plus walimu wengine kwa ujumla kwa nini Serikali isiangalie uwezekano Wa kuwapa fursa nyingine za juu zaidi ili wazidishe jitihada na kuonyesha ufanisi zaidi ktk utendaji wao kama Motisha kwa watumishi Wa uma wengine?

Any ways, Hongereni sana walimu Wa Kisimiri Shule ya Sekondari kwa jitihada zenu za kipekee zilizofanya Shule yenu iongoze nchi nzima katika matokeo ya kidato cha sita Mwaka 2019. Naamini Mh. JPM kupitia wasaidizi wake katika idara ya elimu watawatazama kwa jicho la tatu. Nimewaza sana nikaona si kitu rahisi na kawaida kwa Shule kushika nafasi ya kwanza kwa nchi nzima pasipokuwa na jitihada na moyo Wa kipekee Wa kufanya kazi.
 
Hii shule ina dahiri wanafunzi...wenye division 1 tu...na mwenye combination za point 3 kwanini wasifanye vizuri???
Kuna vitu vingine sio vya kusifia sana
Unamaanisha Serikali inawapendelea au? Mana wanafunzi hao hupelekwa na Serikali hapo. Kwa hyo Hoja yako ni dhaifu kama bunge
 
Hii shule ina dahiri wanafunzi...wenye division 1 tu...na mwenye combination za point 3 kwanini wasifanye vizuri???
Kuna vitu vingine sio vya kusifia sana
Walimu wapo vizuri sana kwenye kuweka wanafunzi kuwa na nidhamu, Mimi nimemaliza pale pia. Kuna mwalimu tulikuwa tunamwita ndugu Binti alikuwa mtaaluma, na mwalimu mwingine peter wa language. Hao walimu kuja kuwaamsha bwenini saa 11 na fimbo muende darasani mkasome ilikuwa ni kitu Cha kawaida kiasi kwamba tulizoea.
Ingawa tulikuwa tunapata muda mwingi sana wa kusoma katikati ya wiki maana walimu hasa wa PCM walikuwa wanafika weekend tu. Yani ijumaa to jumapili lakini ndani ya hizo siku chache tunafundishwa mambo mengi sana kuanzia jtatu ni kureview tu na discussion. Mwalimu wa hesabu Teacher Raymond kila jumamosi mtihani paper 1&2.
Ingawa pia PCM wote tulikuwa na division one kutoka o level ingawa watu wa HKL wenyewe walikuwa mpaka division 3 wapo ila wanapikwa mpaka mtu akipata division 1 ya point 7 ndo anakuwa wa mwisho.
Kwa hiyo mtoa mada yupo sahihi sana, walimu kusema kweli walikuwa na juhudi kufundisha wapewe maua yao tu
 
Back
Top Bottom