Watumishi kutemwa kwenye ajira za Sensa 2022 ni jambo la afya sana

Watumishi kutemwa kwenye ajira za Sensa 2022 ni jambo la afya sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Tuwe na huruma ndugu zangu, tusiwe na mioyo migumu kama korosho.

Maelfu ya vijana wapo mtaani hawana ajira, wewe mtumishi wa umma , sekta binafsi ama uliye na biashara zako unang'ang'ana kuomba hizo ajira za muda mfupi (Siku 21 hadi 35)! Huna aibu?

Serikali imefanya jambo jema sana. Watumishi wa umma wengi wametemwa kwenye ajira za Ukarani, TEHAMA au hata wale wakufunzi. Safi mno.

Wewe unalipwa mshahara (let say 700k), kuna watu wana Masters, Degree, Diploma maelfu na maelfu na ni miaka na miaka wapo mtaani wanasugua gaga, unataka hizihizi ajira?! Huna akili.
 
Bila ya kuzingatia ubora wa kazi unaotakiwa, na kuwapa kazi Four Failures kisa tu hawana ajira tusilalame Sensa itakavyokuwa imeharibiwa.

Kuhoji wenye Kaya na kujaza lile dodoso si kazi lelemama; kisha kutuma kazi kwa njia ya mtandao.

Kwa maoni yangu, watu wenye uelewa fulani kama angalau Ufaulu daraja la III wanahitajika ili kuipa hadhi kazi husika na Elimu
 
Tuwe na huruma ndugu zangu, tusiwe na mioyo migumu kama korosho.

Maelfu ya vijana wapo mtaani hawana ajira, wewe mtumishi wa umma...
Kabla hawajachujwa nilipopata habari kuwa watumishi wameomba nikashauri serikali ipige chini wote waloajiriwa kwani kuwapa watumishi kazi hiyo ni kuzidi kuchochea chuki kati ya wasoajiriwa na serikali,waajiriwa na wasoajiriwa.

Ni uzembe serikali kumpa nafasi muajiriwa na kupoteza muda na hela.Yani atakuwa nje ya eneo aloajiriwa karibu mwezi halafu mwisho wa mwezi analipwa mshahara wote na wa sensa anapata.Serikali piga chini hapo waajiriwa wanaacha pengo kazini kwao kwa uzembe au vinginevyo kata mshahara mana ulafi.
 
𝗡𝗮𝘂𝗺𝗶𝗮 𝘀𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗶𝗺𝗲𝘁𝗲𝗺𝘄𝗮,
 
bd2867fe204344a29933fdc03ce9155e.jpg
 
Mtumishi pia anatafuta pesa nje ya mshahara,Hivo sio dhambi.Hii KAZI ni ya yeyote mwenye vigezo ndio maana usaili umefanyika nchini kote.
 
Tuwe na huruma ndugu zangu, tusiwe na mioyo migumu kama korosho.

Maelfu ya vijana wapo mtaani hawana ajira, wewe mtumishi wa umma , sekta binafsi ama uliye na biashara zako unang'ang'ana kuomba hizo ajira za muda mfupi (Siku 21 hadi 35)! Huna aibu?

Serikali imefanya jambo jema sana. Watumishi wa umma wengi wametemwa kwenye ajira za Ukarani, TEHAMA au hata wale wakufunzi. Safi mno.

Wewe unalipwa mshahara (let say 700k), kuna watu wana Masters, Degree, Diploma maelfu na maelfu na ni miaka na miaka wapo mtaani wanasugua gaga, unataka hizihizi ajira?! Huna akili.
Hakika watuachie nafas kidg ya kulamba asali ya nchi
 
Back
Top Bottom