Watumishi kutemwa kwenye ajira za Sensa 2022 ni jambo la afya sana

Watumishi kutemwa kwenye ajira za Sensa 2022 ni jambo la afya sana

... Wewe unalipwa mshahara (let say 700k), kuna watu wana Masters, Degree, Diploma maelfu na maelfu na ni miaka na miaka wapo mtaani wanasugua gaga, unataka hizihizi ajira?! Huna akili.
Si huwa mnaponda walioajiriwa serikalini, leo vipi tena! Ngoja tukomae nao, hakuna kuachia nafasi kwa mtu anayekukebehi
 
Shida ya jobless hawaaminiki akiharibu kazi utampata wapi? Kuna halmshauri fulani waliweka hao vijana jobless na UVCCM wakaharibu kazi kwenye anwani za makazi matokeo yake Hiyo halmshauri ikaja kuwapigia goti walimu waje wamalizie kazi iliyowashinda hao majobless na UVCCM sasa unadhani halmshauri Hiyo itarudia tena hilo kosa?
 
Tuwe na huruma ndugu zangu, tusiwe na mioyo migumu kama korosho.

Maelfu ya vijana wapo mtaani hawana ajira, wewe mtumishi wa umma , sekta binafsi ama uliye na biashara zako unang'ang'ana kuomba hizo ajira za muda mfupi (Siku 21 hadi 35)! Huna aibu?

Serikali imefanya jambo jema sana. Watumishi wa umma wengi wametemwa kwenye ajira za Ukarani, TEHAMA au hata wale wakufunzi. Safi mno.

Wewe unalipwa mshahara (let say 700k), kuna watu wana Masters, Degree, Diploma maelfu na maelfu na ni miaka na miaka wapo mtaani wanasugua gaga, unataka hizihizi ajira?! Huna akili.
Duniani hatuishi kwa huruma kijana,pambana,unaweza ukawa unamuona ana kazi ila hujui changamoto zake pia,kipato hakijawahi kutosha siku zote,ww jiandae kupambana nao siyo kutia huruma,huruma haijawhi kuwa jawabu,dunia ya leo atakayekuonea huruma ni mzazi wako tu!
 
Kwanza mm kama muajiri chaguo lingekuwa watumishi wa umma,sababu wana anuani za kuelwweka na ni rahisi kuwawajibisha wakikosea!
 
Nunga mkono hoja. Watu wasio na ajira ya kudumu wapewe ajira hiyo ya muda mifupi. Kwanini wenye mishahara yao kila mwezi, waongezewe ajira nyingine? Ni jambo la busara na hekima kuwafikiria pia wasio na ajira angalao wapewe ajira hiyo ya muda mifupi. Nao pia wana haki ya kuonja keki ya taifa. Kinyume cha hapo nitaishangaa serikali hii
 
Ipo hivi vijana wenzangu, ni MUHIMU SANA kutambua DUMIA HAINA HURUMA. Hii ni Dunia ya kibepari zaidi, you don't expect "huruma" na uje kutoboa. Muhimu sana tuwe aggressive na tuendelee kupambana kwelikweli.

Hakuna asiyependa pesa. Mfano mzuri wa wapambanji Afica hii ni Nigerians na jirani zetu wa Kenya hapo. Ukisikia nafasi wewe pamba kadri ya uwezo wako huruma hazitusaidii. Survival of the fittest and struggle for existence is real in this capitalist world! Kupitia ajira za sensa nimepata wazo kubwa la vijana tujiunganisha nguvu na tupambane, nitakuja nalo hapa tulichakate!!

Good luck kwa yeyote aliyeomba ajira ya sensa awe ameajirowa au hana ajira!
 
Mtoa mada nadhani upiganie zaidi waliojipa vyeo na kazi zaidi ya moja, upiganie zaidi wanaoajiri kwa kuangalia uzoefu ili uwaokoe hao vijana, ukishindwa hilo basi hizi nafasi aacha apate yeyote atakayebahatika, maana na wao watasema hilo ni zoezi la mara moja Kila baada ya miaka kumi utapelekaje watoto wasiopevuka kwenye kazi wakiharibu mpaka miaka kumi tena.

Mi naona acha wachangamane fresher na wakongwe kazini wapeane uzoefu.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom