Watumishi mnaohamia private kutoka Serikalini mnahujumu uchumi

Watumishi mnaohamia private kutoka Serikalini mnahujumu uchumi

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,086
Kwenu watumishi mnaoajiriwa bila hata kufanya interview. Watumishi mnaopangiwa vituo vya kazi na serikali kama wanafunzi wanao jiunga kidato cha kwanza kupitia elimu bure. Kisha mnaanza kuleta kiburi na kutelekeza vituo vya kazi kwa kuhamia private mkidai kwamba serikalini hakuna maslahi mazuri. Kwani mlipokua mnaomba hizo kazi mwanzoni hamkujua kwamba serikalini hakuna maslahi mazuri? Kwanini hamkufanya maamuzi mapema ya kuomba hizo kazi private moja kwa moja.

Hivi mnajua serikali inatumia fedha kiasi gani wakati wakufanya mchakato wa kuajiri. Hamwoni kwamba mnairudisha nyuma serikali kwa kuanza kutenga fedha zingine kwaajili ya kuaajiri watumishi wengine ili wazibe hayo mapengo yaliyo achwa na ninyi. Hamwoni kwamba mnaingiza serikali hasara mara mbili. Hamwoni kwamba mnaipa serikali mzigo wa kuanza kuwaza kutenga fedha zingine. Hamwoni kwamba mnaingiza serikali kuwa na upungufu wa watumishi wa umma. Hamwoni kwamba mnaharibu kodi zetu.

Mimi leo nawaita ni wahujumu uchumi wa nchi.

Mfano;
Madaktari wakiwa na uhitaji wa ajira wanalialia mitandaoni, kisha serikali inawapatia ajira tena bila interview wala kutuma barua za maombi. Ni kwamba wanapangiwa vituo vya kazi kama wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kwa kupitia elimu bure. Hawafanyishwi cha usaili wala nini. Wakisha pata ajira tu wanaanza usumbufu na kutelekeza vituo vyao vya kazi huku wakisema mara oooh maslahi ni madogo.

Sasa kwanini hukuchagua kufanya kazi private tangia mwanzo. Kwanini uisumbue serikali kuanza kuajiri mtumishi mpya wakati unaona kabisa serikali inatumia pesa nyingi sana wakati wa kuajiri mfanyakazi. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za serikali na ni uhujumu uchumi. Hata mimi sikubaliani na watumishi wanaohamia private wanaisumbua serikali kuanza kuajiri kila wakati.

Hivyo naungana na Rais Magufuli kuwaadhibu wanaotelekeza vituo walivyo pangiwa. Kama mtumishi hutaki kazi ya serikali usiisumbue serikali kuanza kukuajiri wakati unaona moyo wako unakushawishi kuikimbia kazi hiyo baadaye. Kwanini hiyo kazi usiwaachie wengine wenye uhitaji wa kazi hiyo. Huo ni ubinafsi mkubwa kwanini usiende private tokea mwanzo kwani ulikatazwa? Nenda private waachie kazi wengine kwasababu unaingiza serikali hasara tu. Fedha zinatengwa tunakuajiri na tunakupatia fedha zetu kwaajili ya kwenda kuanzia maisha huko alafu unatelekeza kituo cha kazi. Huo ni uhujumu uchumi.
 
Umeishia darasa la ngapi mkuu?

Mana hujui hata "greener pasture" kwa mfanyakazi
 
Aisee

Hii thinking ni very very dangerous....

JF ondoeni huu uzi,pleaseeee

Seriously
Mimi ni mlipa kodi kama wewe kama na wewe ni mmojawapo unahujumu uchumi na kuipa serikali kuirudisha serikali nyuma ni bora uache au kama ulikua na mpango sitisha. Ninyi ndio mnasababisha allocation ya employment inakua ni mbovu. Mnapangiwa vituo kisha mnakimbia.
 
Magufuli aliacha chaki akakimbilia siasa. Je na yeye arudishwe kwenye ualimu?
 
Nini sababu ya wao kuhama?

Ukitatua hiyo sababu wote utawaona wametulia walipo.
 
Back
Top Bottom