elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Watumishi na viongozi wa umma, hasa wa wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi wameobwa waige na kufuata nyayo za Rais Dkt John Magufuli za katika kushughulikia kero za kijamii.
Mzee Mohamed Auko (80) ambae ni miongoni mwa wafanyabiashara ndogondogo katika soko hilo alisema watendaji na viongozi hawana budi kuiga mwenendo wa utendaji wa Rais Dkt John Magufuli katika kushughulikia kero na matatizo ya wananchi badala ya kutenda tofauti.
"Tunavujiwa mvua, soko bovu tumelalamika hatusikilizwi, tunapata hasara bidhaa zinanyeshewa sasa miaka minne. Tunahangaika wakati tunalipa ushuru, mvua ikinyesha tu maji yanajaa. Hawa wanajifunza na kuiga kwa nani? Rais Magufuli mbona ni mchapakazi na anachukua hatua kushughulikia changamoto bila kuchelewa?,'' alihoji mzee Auko.
Mzee huyo anaetambulika kama sharifu alisema iwapo viongozi na watendaji wa umma wataiga utendaji na uongozi wa Rais Magufuli nchi itabadilika haraka kiuchumi na maendeleo kwa kipindi kifupi.
Kuonesha amemkubali Rais Magufuli mzee huyo alisema kwa kipindi kifupi cha uongozi wake(miaka minne) amefanya mambo makubwa nchini.
''Asiyemshukuru na kumpongeza ana lake, barabara ya Kwamkocho hadi Kivinje haikuwahi kujengwa tangu mkoloni. Lakini Magufuli amejenga, tena kwa lami, umeme, zahanati, hosipitali na mambo mengi yanafanyika. Ukienda Pande, Lihimalyao, Ntitimila, Ntandula, Malalani hata Ntonga kuna mabadiliko makubwa. Pande wanakituo cha afya, yote ni kazi ya muda mfupi ya Magufuli,'' alisitiza mzee Auko.
Mzee huyo alitoa wito kwa mkurugenzi mtendaji na mwenyeki kiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa wawe mfano wa kuiga utendaji na uongozi wa Rais Magufuli kwa kukaribati haraka jengo hilo ili kuwanusuru na hasara wanazopata.
Maelezo ya mzee Auko yaliungwa mkono na mchuuzi wa nyanya katika soko hilo, Marimu Kajoka aliyesema soko hilo ni bovu linawatia hasara. Yeye amewahi kupata hasara kutokana na nyanya zake tenga tatu kuoza baada ya kunyeshewa mvua zikiwa ndani ya jengo hilo.
Alisema yanayofanywa na Rais Magufuli nitofauti na yanayofanywa na watendaji na viongozi wa umma walio ngazi za chini.
Muungwana Blog ilimtafuta na kumpata mkurugenzi mtendaji ( DED), Renatus Mchau ambaye Mchau alikiri kwamba soko hilo linahitaji ukarabati, na tayari alishawaagiza wataalamu wa idara ya ujenzi kwenda kufanya tathimini ili kujua kazi zilizopo, aina na idadi ya vifa na kiasi cha fedha kinachohitajika kwa ukarabati huo.
Alisema kilichochangia kuchelewa kufanyika ukarabati huo ni marekebisho mengine katika eneo muhimu ambalo ni kituo cha mabasi cha hapo Kilwa Masoko. Kwahiyo ilibidi wamalize matengenezo hayo ndipo wahamie kwenye matengenezo ya soko.