kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
BAADHI ya wafanyakazi wa Benki ya NBC,Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam, wamedai kudhalilishwa na mabosi wao kwa kuvuliwa nguo zote.Wakizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, wafanyakazi hao walisema walifanyiwa hivyo Ijumaa iliyopita.
Tukio la wafanyakazi hao kufanyiwa unyama huo, tayari limeripotiwa polisi na kupewa kumbukumbu namba CD/RB/4073/2011 na CD/IR/1319/2011.
Mmoja wa wafanyakazi hao, Michael Matayo, alisema wafanyakazi waliofanyiwa udhalilishaji huo ni watano na kwamba ni wale wa kitengo cha usafirishaji fedha.Alisema siku ya tukio, walikuwa wanajiandaa kwenda kula na kwamba kabla ya kutoka lazima upite mageti matatu na kukaguliwa na mlinzi.
"Tulipofika geti la mwisho meneja wetu alituita akatuuliza mnajua tunachotaka kufanya, tukamwambia hatujui akasema tumsubiri nje,"alisema Matayo.Alisema baadaye waliitwa na kuingia chumba cha kubadilishia nguo chenye kamera ya CCTV na kwamba baada ya kutoka kwenye chumba hicho waliingia katika chumba kingine ambacho hakina kamera ya CCTV na kuanza kusachiwa.
Mfanyakazi mwingine aliyedai kudhalilishwa ni Ramadhan Mbwana, ambaye alisema kitendo hicho, kilidumu kwa dakika 20 na kwamba waliamriwa kuvua nguo zote na kubaki uchi na kuchuchumaa.
Alisema unyama huo ulifanywa na Mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji Fedha katika benki hiyo ambaye ni raia wa Ghana."Baada ya kutusachi na kuridhika kuwa hatujaiba hela alituachia,"alisema Mbwana.
Wafanyakazi hao pia walidai kuwa Machi 19 mwaka huu, walifanyiwa udhalilishaji mwingine ambapo waliamriwa kunyanyua mikono juu kwa zaidi ya nusu saa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kusachiwa.
Licha ya kuvuliwa nguo, wafanyakazi hao wamesema wamekuwa wakinyanyaswa kwa kutukanwa kudharauliwa na kufanyishwa kazi kwa muda mrefu.Hata hivyo, Meneja Uhusiano wa benki hiyo Robi Matiko,alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, aikiri kuwa na taarifa kuhusu tukio hilo lakini alisema hawezi kuzieleza kwa undani zaidi kwa sababu hawajapata taarifa kamili.Uongozi wa NBC makao makuu nao ulisema hauna taarifa.