KERO Watumishi Nzega DC tunaomba kupewa Barua zetu za kuthibitishwa kazini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
HABARI JAMII FORUM.

Poleni na majukumu naomba utupazie sauti sisi Watumishi wa Nzega DC tumeajiriwa tangu mwaka 2024 ila mpaka leo tunazungushwa kupewa barua zetu za uthibitisho tumemuuliza mpaka Mkurugenzi hatupi majibu ya kueleweka walisema mpaka Baraza la Madiwani likae ndio watuthibitishe na madiwani wamekaa kikao tangu wiki iliyopita lakini tumeambiwa bado tusubirie.

Sasa kwa hali hii hata morali ya kufanya kazi inakuwa inashuka sana kwa nini ishu ya kupewa barua ya kuthibitishwa kazini inakua ngumu hata kama umekidhi vigezo vya kuthibitishwa???

Tunaomba msaada wa kutupazia sauti.

AHSANTE
 
Unataka uthibitishwe ili ufanye nini? Kama unachotaka kufanya ni mpaka ESS ione 'cofirmation date' hutakiwi kugombana wala kuja kuanzisha uzi JF.

Mwambie HR unachotaka so atakujazia kwenye mfumo ili confirmation date isome kwenye mfumo. So utaendelea na mambo yako wakati unasubiri hiyo barua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…