A
Anonymous
Guest
Sisi watumishi wa TTCL Corporation tunakabiliwa na changamoto kubwa licha ya kutekeleza majukumu yetu kwa bidii na kujaza taarifa za utendaji kazi kwenye mfumo wa ESS Utumishi (PEPMIS) kama inavyotakiwa.
Tatizo linalotusumbua ni kwamba baadhi ya viongozi wetu, hususan Mameneja, hawapitishi tathmini za utendaji kazi ambazo tumekuwa tukiziwasilisha kwenye mfumo huo kwa wakati. Hali hii imekuwa na athari kubwa kwa watumishi wengi.
Kwa mfano, mwaka jana baadhi ya watumishi walikosa fursa ya kupandishwa vyeo kutokana na kutotimiza vigezo vinavyohitajika kwenye mfumo. Ili mtumishi aweze kustahili kupandishwa cheo, anatakiwa kuwa na kiwango cha utendaji kisichopungua asilimia 75. Hata hivyo, baadhi ya watumishi walikuwa wamejaza taarifa zao kikamilifu kwenye mfumo, lakini tathmini zao hazikupitishwa na Mameneja wao, jambo lililosababisha waonekane hawajakidhi vigezo vinavyohitajika.
Kwa sasa tunaona dalili za hali hiyo kujirudia tena mwaka huu. Baadhi yetu tumeshajaza taarifa za utendaji kazi kwa muda mrefu, lakini hadi sasa hazijapitishwa na viongozi husika.
Tunaiomba mamlaka inayohusika kuingilia kati suala hili ili kuhakikisha tathmini za watumishi zinapitishwa kwa wakati na kuepusha athari zinazoweza kujitokeza, ikiwemo kukosa stahiki za kupandishwa vyeo kutokana na sababu zisizotokana na uzembe wa watumishi wenyewe.
Asante.