KERO Watumishi tuliohama Hospitali ya Wilaya ya Nzera - Geita hatujalipwa malipo ya 'extra duties'

KERO Watumishi tuliohama Hospitali ya Wilaya ya Nzera - Geita hatujalipwa malipo ya 'extra duties'

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kutokulipwa malipo ya extra duties kwa watumishi ambao tumehama katika Hospitali ya Wilaya ya Nzera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mkoa wa Geita.

Viongozi wa hospitali hawajalipa malipo ya extra duties kwa wafanyakazi ambao tulifanya kazi hizo kwa nguvu zetu zote. Badala yake, wamelipa wafanyakazi waliopo kazini kwa sasa. Hii si haki kwa sababu wote tulitakiwa kulipwa malipo hayo, hata kama tumehama, kwa kuwa tulifanya kazi hizo. Malipo hayo ni ya kuanzia mwezi wa 10 hadi mwezi wa 12 mwaka 2025, na tuliahidiwa kulipwa lakini mpaka sasa hatujalipwa.

Tupo wengi ambao tumeathirika na suala hili. Mrejesho tulioupata ni kwamba fedha hazitoshi, hivyo zimeelezwa kutosha kuwalipa waliopo kituoni pekee, huku waliokwisha hama tukiachwa. Wengine tulihama mwezi wa 4, 6 na 8 mwaka huu, mimi binafsi nilihama mwezi wa 8.

Naomba wahusika walisaidie suala hili ili tulipwe stahiki zetu za extra duties tulizofanya.
 
Back
Top Bottom