A
Anonymous
Guest
Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), hususan wanaofanya kazi katika mradi wa SGR, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutolipwa madai yao kwa muda mrefu, kuanzia kipindi cha ujenzi hadi hatua ya uendeshaji wa reli.
Watumishi wengi hutumwa kufanya kazi nje ya vituo vyao, lakini hawalipwi stahiki zao kwa wakati. Wapo wanaodai malipo yaliyodumu zaidi ya miaka miwili au mitatu. Kila wanapofuatilia Idara ya Fedha huambiwa kuwa shirika halina fedha za kulipa madeni hayo.
Kinachoshangaza ni kwamba madai mengine, hata ya kiasi cha takribani shilingi 400,000, hubaki bila kulipwa hadi mwaka wa fedha unaisha, huku fedha zikirejeshwa serikalini kwa madai ya kutotumika. Hali hii imewaacha watumishi wakijiuliza kwa nini fedha za stahiki zao hazipewi kipaumbele.
Ni kweli watumishi hulipwa mishahara yao, lakini malipo ya posho na madai mengine yamekuwa tatizo sugu. Mara nyingi mtumishi hutumwa kikazi kwa kutumia fedha zake mwenyewe, na anapofuatilia malipo baada ya kurejea huambiwa asubiri. Wakati mwingine posho hizo hazilipwi kabisa.
Pia kuna malalamiko kuhusu utendaji wa Idara ya Fedha. Inadaiwa kuwa viongozi wa idara hiyo, kuanzia Mkurugenzi wa Fedha na wasaidizi wake, huidhinisha malipo lakini fedha hazitolewi hadi mwaka wa fedha unapomalizika. Licha ya watumishi kuendelea kuwasilisha madai yao kila mwaka, hakuna hatua za maana zinazochukuliwa kuyalipa.
Kwa sasa, wapo watumishi ambao bado wanadai malipo ya mwaka 2022, 2023, 2024 na hata 2025. Hali hii inaonekana kuwa na viwango tofauti vya utekelezaji, kwani viongozi wakuu hulipwa fedha za safari na kazi zao kabla ya kuondoka, ilhali watumishi wa kawaida hulazimika kusubiri kwa miaka bila mafanikio.
Inadaiwa pia kuwa Idara ya Rasilimali Watu (HR) inafahamu changamoto hii, lakini hadi sasa haijapatiwa suluhisho la kudumu. Watumishi wengi wanaona hali hii ni mfano wa matumizi ya viwango tofauti (double standards) katika utekelezaji wa haki na stahiki za wafanyakazi.