KERO Watumishi wa Afya Halmashauri ya Nyang’hwale - Geita hatujalipwa Fedha za Kujikimu, wanatuzungusha tu

KERO Watumishi wa Afya Halmashauri ya Nyang’hwale - Geita hatujalipwa Fedha za Kujikimu, wanatuzungusha tu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
JamiiForums tunaomba mtusaidie kupaza sauti Watumishi wa Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang`hwale, ajira za August 2025 na January 2026 mpaka leo hatujalipwa fedha zetu za kujikimu licha ya kuambiwa hizo fedha kutolewa na Serikali tangu Juni 2026.
 
Watumishi ajira Mpya wilaya ya Nyangh'wale-Geita tulio ajiliwa mwaka jana hatujalipwa fedha ya kujikimu mpaka sasa, tukiuliza kwa viongozi hatupewi majibu yanayoeleweka juu ya lini au kama tutalipwa fedha hiyo na pia tukiuliza sana wapo wakubwa wanatoa kauli za vitisho kwamba si tunalipwa mshahara kana kwamba hatustahili fedha hiyo, Maisha ni magumu kwa mtu kuanza maisha eneo ambalo haukuwa ukiishi awali.
 
Hatujalipwa hela zetu za kujikimu ikiwa Tamisemi walishazileta na kutoa amri zitolewe kabla ya June kuisha, tukifatilia kwa wakuu wa idara na wahusika tunazungushwa hakuna jibu lolote la kueleweka wanatupa zaid zaid ni vitishoo
 
Halmashauri ya Nyang’hwale kundi la mwisho limelipwa hela zao za kujikimu leo 🙏
 
Back
Top Bottom