A
Anonymous
Guest
Sisi watumishi wa afya tulioajiriwa mwezi Novemba, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Kilimanjaro tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie suala la kuthibitishwa kwetu kazini, kwani mpaka sasa hatujapatiwa barua za kuthibitishwa wala barua za kuongezewa muda wa probation period.
Kutokana na hali hiyo, watumishi wengi tumebaki katika sintofahamu bila kujua hadhi yetu ya kiutumishi ipo katika hatua gani?
Tunaelewa kuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu za Utumishi wa Umma, mtumishi anatakiwa kuthibitishwa baada ya kukamilisha probation endapo amekidhi vigezo vilivyowekwa, na iwapo hajakidhi anatakiwa kupewa taarifa rasmi ya kuongezewa muda wa probation pamoja na sababu husika.
Hivyo, tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie suala hili ili watumishi waliokidhi vigezo wapatiwe barua za kuthibitishwa kazini, na wale ambao bado hawajakidhi vigezo vya kuthibitishwa wapatiwe taarifa rasmi ya extension ya probation kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.