A
Anonymous
Guest
Tunaomba msaada wa kutupazia sauti sisi Watumishi wa Ajira Mpya wa Januari 2026 wa Kada ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida, ambao hadi sasa hatujapatiwa fedha za kujikimu licha ya taarifa kuwa fedha hizo zimeshawasilishwa kutoka Hazina kwenda Halmashauri.
Kwa muda sasa tumekuwa tukifuatilia stahiki hizi kupitia njia mbalimbali, lakini badala ya kupata majibu ya kuridhisha, baadhi yetu tumekuwa tukikumbana na vitisho vya kuhamishiwa katika vituo vya mbali vya vijijini pale tunapoulizia haki zetu.
Aidha, kumekuwa na hatua za kuwaondoa baadhi ya watumishi wapya katika makundi ya mawasiliano baada ya kuibua hoja kuhusu fedha za kujikimu.
Fedha za kujikimu ni stahiki muhimu kwa watumishi wapya ili kuwasaidia kuanza maisha na majukumu katika vituo vyao vya kazi. Kutopatiwa fedha hizo kwa wakati kunasababisha ugumu mkubwa wa maisha na utekelezaji wa majukumu ya kikazi.