A
Anonymous
Guest
Habari, nawasilisha malalamiko haya kwa niaba ya watumishi wa Bunda DC.
Kwa kawaida, watumishi tumekuwa tukipokea posho za masaa ya ziada kila mwezi, fedha ambazo hutolewa na Hazina kwa ajili ya kuwalipa watumishi wanaostahili. Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, hadi sasa hatujapokea posho ya mwezi wa Julai.
Taarifa tulizonazo zinaeleza kuwa fedha hizo zilifika kutoka Hazina, lakini badala ya kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, zilipelekwa kugharamia shughuli za kukimbiza Mwenge wa Uhuru uliopita katika Halmashauri yetu tarehe 9 Agosti.
Hali hii imetufanya tujiulize: Je, Serikali haina fedha za kugharamia shughuli za Mwenge kiasi cha kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya watumishi? Kwa nini haki za watumishi ziathiriwe kwa ajili ya shughuli nyingine?
Mishahara ya watumishi wengi ni midogo, hivyo posho hizi za masaa ya ziada zimekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na changamoto za maisha. Kwa baadhi ya watumishi, hakuna chanzo kingine cha kipato zaidi ya mshahara na posho hizo.
Aidha, Halmashauri ina mapato yake ya ndani. Tunaomba kuelewa kwa nini fedha hizo hazikutumika kugharamia shughuli za Mwenge, badala ya kutumia fedha zilizotengwa kwa ajili ya watumishi.
Tunaomba Serikali ilichunguze suala hili na kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya watumishi zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa. Hali hii inawaumiza watumishi na imeanza kuathiri hata morali na hamasa ya kufanya kazi.
Naomba kuwasilisha.