A
Anonymous
Guest
Watumishi katika Idara ya Sekondari ya Halmashauri ya Tarime Vijijini hatujalipwa fedha za likizo kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.
Baadhi ya watumishi bado wana madai ya fedha za likizo za miaka iliyopita bila kupatiwa ufumbuzi. Wakati mwingine malipo yanapotolewa, hayalingani na kiasi kinachostahili kulipwa na hakuna maelezo yanayotolewa kuhusu tofauti hiyo.
Kwa mfano, mtumishi anaweza kuwasilisha maombi ya fedha za likizo yenye thamani ya Shilingi 500,000 kulingana na vigezo, lakini akalipwa Shilingi 100,000 pekee bila ufafanuzi wowote.
Aidha, kuna madai mengine ya stahiki za watumishi ambayo yamekuwa hayapatiwi utekelezaji. Watumishi wanaomba mamlaka husika kufuatilia suala hili na kuhakikisha wanapatiwa haki zao kwa mujibu wa taratibu.
Pia soma ~ Naibu Waziri Qwaray: Waajiri wote lazima watenge bajeti ya kumlipa mtumishi pindi anapohama