KERO Responded Watumishi wa Mamlaka ya Maji Igunga (IGUWASA) tunaomba ufanyike uchunguzi dhidi ya ofisi yetu, mambo hayapo sawa

KERO Responded Watumishi wa Mamlaka ya Maji Igunga (IGUWASA) tunaomba ufanyike uchunguzi dhidi ya ofisi yetu, mambo hayapo sawa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Screenshot 2026-06-05 105652.jpg

OMBI LA UCHUNGUZI WA HARAKA KUHUSU IGUWASA​

Tunaziomba Wizara ya Maji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mheshimiwa Waziri wa Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAKUKURU na mamlaka nyingine husika kufanya uchunguzi wa kina katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) kutokana na malalamiko na wasiwasi unaoendelea kujitokeza miongoni mwa watumishi na wadau wa taasisi.

Kumekuwa na madai kuhusu usimamizi wa rasilimali za taasisi, matumizi ya fedha za umma, utoaji wa safari za kikazi, upandishaji wa madaraja na ucheleweshaji wa stahiki za watumishi.

Aidha, kuna malalamiko kuhusu:
• Ucheleweshaji wa mishahara, rejesho na malipo ya vibarua.
• Kutolipwa stahiki za safari za kikazi kwa muda mrefu.
• Upungufu wa vifaa vya kazi.
• Madeni ya taasisi (NHIF, PSSF, TRA na wazabuni).
• Kuondolewa kwa Mhasibu na Mkaguzi wa Ndani kwa wakati mmoja.
• Malipo kutopitia mifumo rasmi ya serikali.
• Miradi mbalimbali na matumizi yake.
• Matumizi ya petty cash.
• Changamoto za Idara ya HR.
• Upendeleo katika safari za kikazi.
• Mahusiano ya karibu katika maamuzi ya kiutawala.
• Matumizi ya fedha kutanguliza maslahi binafsi.
• Maamuzi ya kifedha kufanyika bila kufuata taratibu rasmi.

Tunaiomba Wizara ya Maji, Katibu Mkuu, Waziri wa Maji, Ofisi ya Waziri Mkuu na TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na: Watumishi na Wadau Wanaojali Maendeleo ya IGUWASA

Ufafanuzi ~ IGUWASA yatoa ufafanuzi kuhusu hoja ya Mdau aliyehoji utendaji wa Mamlaka hiyo
 
Back
Top Bottom