KERO Ucheleweshaji Malipo ya Mishahara - Watumishi wa MSF Chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale

KERO Ucheleweshaji Malipo ya Mishahara - Watumishi wa MSF Chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Liwale

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa unyenyekevu mkubwa tunapenda kutoa kero yetu sisi watumishi wa MSF - Medecins Sans Frontieres tunaofanya kazi chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi

1. Hali ilivyo sasa
Hadi leo tarehe 5/04/2026 mishahara yetu bado haijapatikana. Ucheleweshaji huu umetufikisha pabaya sana. Wenzetu wapya walioajiriwa mwezi huu ni mwezi wao wa kwanza, maskini hawana hata mtaji wa kujikimu, lakini bado wanasubiri mshahara. Pia kwa sasa shule zimefunguliwa na wengi wetu tuna majukumu ya ada, mahitaji ya watoto na familia.

2. Chanzo cha kero
Kwa sasa mishahara yetu inapitishwa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Halmashauri ilituahidi kuwa itafuatilia malipo yawe kwa wakati ili tuweze kutekeleza majukumu yetu bila kikwazo. Kwa bahati mbaya, halmashauri ndio chanzo cha tatizo maana shirika linafanya kila kitu kwa wakati lakini halmashauri ndio inayotuumiza

Tunashuhudia kuwa MSF kama shirika linatimiza majukumu yake kwa wakati na linafanya kazi kubwa ya kuwahudumia jamii ya Liwale na maeneo jirani. Ndio maana kwa unyenyekevu tunapendekeza: Kama kuna uwezekano, mishahara yetu ilipwe moja kwa moja na MSF kama ilivyokuwa awali. Hii itaondoa urasimu na kutoa uhakika wa malipo.

3. Swali letu kwa heshima
Tunajiuliza tu kwa unyenyekevu: Kama watumishi wa halmashauri waliamua pesa yetu ipitie Halmashauri ya Liwale, je kama wao watumishi wa Halmashauri wenyewe wangekuwa wanacheleweshewa mishahara kila mwezi hivi na Serikali, wangevumilia vipi ?au wanafanya maamuzi hayo kwakua wanaoadhirika sio wenyewe

Sisi tunafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa na kuokoa maisha ya wananchi wa Liwale kwa moyo, lakini tunapokuwa na stress ya kifedha kila mwezi, ufanisi na huduma yetu inapungua.

Tukiomba mazingatie uwezekano wa kurudisha mfumo wa malipo direct kutoka MSF kwenda kwa watumishi, ili tuondoe kero hii ya mara kwa mara.

Hatuna lengo la kulaumu. Tunafahamu kila mmoja ana majukumu yake. Ombi letu ni la kibinadamu tu tulipwe kwa wakati ili tuendelee kuwahudumia wananchi wa Liwale kwa ufanisi zaidi.
 
Kwa unyenyekevu mkubwa tunapenda kutoa kero yetu sisi watumishi wa MSF - Medecins Sans Frontieres tunaofanya kazi chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi

Hadi leo tarehe 6/04/2026 mishahara yetu bado haijapatikana. Ucheleweshaji huu umetufikisha pabaya sana. Wenzetu wapya walioajiriwa mwezi huu ni mwezi wao wa kwanza, maskini hawana hata mtaji wa kujikimu, lakini bado wanasubiri mshahara. Pia kwa sasa shule zimefunguliwa na wengi wetu tuna majukumu ya ada, mahitaji ya watoto na familia.

Kwa sasa mishahara yetu inapitishwa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Liwale. Halmashauri ilituahidi kuwa tutakuwa chini ya usimamizi wao ili tupate stahiki zetu kwa wakati Kwa bahati mbaya, ndio mchakato huo huo umekuwa chanzo cha kuchelewa kila mwezi na wao ndio wanasababisha changamoto hii na kuna baadhi yetu wanalipa nauli karibu 8000 nauli kwenda kazini hii hela tutaitoa wapi

Tunashuhudia kuwa MSF kama shirika linatimiza majukumu yake kwa wakati na linafanya kazi kubwa ya kuwahudumia jamii ya Liwale na maeneo jirani. Ndio maana kwa unyenyekevu tunapendekeza mishahara yetu ilipwe moja kwa moja na MSF kama ilivyokuwa awali. Hii itaondoa urasimu na kutoa uhakika wa malipo.

Tunajiuliza tu Kama uamuzi ulikuwa pesa ya malipo yetu ipitie Halmashauri ya Liwale, je kama watumishi wa Halmashauri wenyewe wangekuwa wanacheleweshewa mishahara kila mwezi hivi na Serikali, wangevumilia vipi au walifanya hayo maamuzi kwakuwa wao haiwaumizi kwa namna yoyote

Sisi tunafanya kazi ya kuwahudumia wagonjwa na kuokoa maisha ya wananchi wa Liwale kwa moyo, lakini tunapokuwa na stress ya kifedha kila mwezi, ufanisi na huduma yetu inapungua.

Tukiomba uwezekano wa kurudisha mfumo wa malipo direct kutoka MSF kwenda kwa watumishi, ili tuondoe kero hii ya mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom