KERO Watumishi wa Shule ya msingi Azimio, Mbeya hatujalipiwa michango ya Bima tangu mwezi Julai

KERO Watumishi wa Shule ya msingi Azimio, Mbeya hatujalipiwa michango ya Bima tangu mwezi Julai

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Baba Bless

New Member
Joined
Mar 27, 2018
Posts
3
Reaction score
2
Sisi ni baadhi ya watumishi wa Shule ya Msingi Azimio, tungependa kulifikisha malalamiko yetu kwa mamlaka husika kuhusu kutolipwa kwa michango yetu ya bima ya afya tangu mwezi Julai, licha ya makato kuendelea kufanyika kwenye mishahara yetu.

Hali hii imetusababishia usumbufu mkubwa, kwani tunapokwenda kupata matibabu sisi au ndugu zetu tunalazimika kulipia gharama za matibabu kwa fedha taslimu (cash) kutokana na bima zetu kutokuwa hai.

Tunaona hali hii si ya haki, kwa kuwa michango ya bima inakatwa kwenye mishahara yetu kila mwezi, lakini fedha hizo haziwasilishwi kwa wakati kwenye mifuko ya bima.

Soma Pia: Bima ya Afya ya Jeshi(JWTZ) haitusaidii Wanajeshi na Familia zetu

Tunaomba mamlaka husika zichunguze suala hili na kuhakikisha michango yote iliyokatwa inawasilishwa kwenye bima zetu ili kurejesha huduma za matibabu. Hatuwezi kuendelea kukatwa fedha kwa ajili ya bima huku sisi na familia zetu tukishindwa kunufaika na huduma tunazostahili.
 
Back
Top Bottom