Watumishi wa Umma kucheka au kulia

Watumishi wa Umma kucheka au kulia

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Waswahili walisema usiku wa deni haukawii kucha. Zimebaki siku chache ili watumishi wa umma nchini waweze kupokea mshahara wao mpya wa mwaka wa fedha 2022-2023.

Kufuatia nyongeza ya 23.3% iliyotangazwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan siku ya Mei Mosi 2022, watumishi wengi wamejawa na matumaini makubwa kuwa mishahara yao itapanda walao kwendana na mfuko wa bei hapa nchini.

Hata hivyo baada ya kutangazwa kwa nyongeza hiyo palitokea mijadala ya hapa na pale kuhusu ongezeko hilo la 23.3%.

Kwa hiyo siku chache zijazo tutegemee watumishi kucheka, kunung'unika au kulia.July Salary-Loading.
 
Back
Top Bottom