Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana2.3.10 Ruhusa ya Masomo
Ruhusa hii hutolewa baada ya mwajiriwa mpya kufanya kazi zaidi ya miaka miwili. Unaweza kuruhusiwa kwenda masomoni baada ya kuomba kuwekwa kwenye mpango wa mafunzo wa Taasisi. Utaweza pia kuomba kugharamiwa na mwajiri au kujigharamia mwenyewe au kuomba ufadhili kupitia Bodi ya Mikopo n.k. Kwa kuwa nia ya masomo ni kukuendeleza kitaaluma, ni vema ukajiendeleza katika fani unayofanyia kazi (proffessional carrier development) [Rejea Kanuni ya G.7(1)(a-j) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].kwa mujibu wa Mwongozo wa Uendeshaji wa Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wa mwaka 2008
Sawa mkuu🙏Kama hujatimiza miaka 3 hiyo ruhusa huwezi kupewa
Kama hujatimiza miaka mi3 mambo matatu HAYAKUHUSU
1. Uhamisho
2. Masomo
3. Kubadilishana.
Baada ya mwaka mmoja ( kuthibitishwa kazini) una haki ya kupewa LIKIZO YA MALIPO.
NB: Labla sa hivi kuna mabadiliko
Hii ni kutokana na TAMISEMI, wizarani labla kuna utaratibu tofauti.
Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
sawa mkuu Asante mno🙏Mkuu,
Mimi binafsi, viongozi wangu waligoma. Nilipostpone masomo nikiwa mwaka wa pili nikaenda kuripoti kazini. Nikaambiwa Hadi ipite miaka mitatu.
So miaka mitatu ilipotimia ndio nikapata Ruhusa. Haijalishi unajisomesha mwenyewe au vipi.
Mimi nilijisomesha mwenyewe lakini kiutaratibu hairuhusiwi Hadi utimize miaka mitatu.
Jaribu kuongea na Kiongozi wako akupe ufafanuzi zaidi.