A
Anonymous
Guest
Kero yangu inahusu baadhi ya watumishi wa umma ambao tumekosa kupandishwa madaraja kutokana na changamoto zinazotokana na matumizi ya mfumo wa PEPMIS na uzembe wa baadhi ya wakuu wa vituo.
Baadhi yetu tulihama vituo vya kazi, lakini taarifa katika mfumo zinaendelea kuonesha vituo vya zamani badala ya vituo tulivyopo kwa sasa. Kutokana na hali hiyo, tathmini za utendaji na majukumu yetu hushindwa kujazwa kwa usahihi, jambo linalosababisha kupata alama za chini zisizoendana na utendaji wetu halisi.
Changamoto kubwa zaidi ni kwamba baadhi ya wakuu wa vituo vya zamani ambako mshahara bado unasomeka kwenye mfumo huwa hawako tayari kushirikiana katika kujaza taarifa zinazohitajika. Wakati mwingine watumishi hulazimika kufuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio, na katika baadhi ya matukio hudaiwa kutoa fedha ili kusaidiwa kukamilishiwa taarifa hizo.
Matokeo yake, watumishi wengi wameathirika katika mchakato wa kupandishwa madaraja na kupata stahiki zao kwa wakati, si kwa sababu ya kutofanya kazi vizuri, bali kutokana na mapungufu ya kiutawala na usimamizi wa mfumo.
Tunaiomba Serikali na mamlaka husika kuingilia kati, kufanya uhakiki wa taarifa za PEPMIS, kuwajengea uwezo wakuu wa vituo kuhusu matumizi sahihi ya mfumo huo, na kuhakikisha hakuna mtumishi anayenyimwa haki zake kutokana na makosa ya kiutawala au vitendo vya rushwa.
Pia soma ~ Prof. Shemdoe: Uzembe wa Ma-Afisa Rasilimali Watu katika Mfumo wa PEPMIS umezuia Watumishi kutopanda daraja