Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,335
- 29,114
Katibu Mkuu Utumishi ametoa maelekezo kuhusu Watumishi wa Umma wanaoshiriki katika mchakato wa kugombea nyadhifa za kisiasa kwamba:-
1. Mishahara yao itaendelea kusimamishwa kwa mwezi Agosti pia.
2. Wawasilishe maombi ya vibali vya likizo bila malipo kwa KM Utumishi (kwa wale ambao ni mameneja) kupitia kwa mwajiri wao. Ambao sio meneja wataomba kwa Msajili wa Hazina
3. Vibali vya likizo bila malipo vitatolewa kwa kipindi cha miezi 2 kuanzia 1/7/2020 hadi 31/8/2020
4. Maombi ya kurejea katika Utumishi wa Umma kwa ambao hatateuliwa yawasilishwe kwa KM Utumishi kupitia kwa mwajiri kuanzia tarehe 25 /8/2020
5. Waajiri wameelekezwa mishahara ya watumishi hao iliyozuiliwa iwasilishwe kwa Katibu Mkuu Hazina.
Kufuatia hali hiyo unaelekezwa kuandika barua upya ya kuomba likizo bila malipo, ukitaja jimbo ulilogombea au viti maalum.
Utajua hujui, tutaelewana tu!