Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Kama cc
Sheria iko wazi wakasome hawajaonewa
Kama ccm ilijua Sheria iko wazi na walikuwa na Nia njema,Kwanini watumishi hawakusomewa Sheria hiyo wakati wanapewa fedha za fomu na michango mbali mbali? Wenye hiyo Sheria tunaomba aiweke haps tuisome.ni uonevu mtupu na njia ya kukatisha tamaa walio Soma kugombea ili wahombeaji wawe wale was darasa la Saba tu.Mfanyabiashara wa mafuta maarufu Hamis Tabasamu hivi karibuni ameshika nafasi ya kwanza kura za maoni CCM jimbo la Sengerema. Hamis Tabasamu mwenye elimu ya darasa la saba tu ameweza kuwashinda wasomi wabobezi wa maswala mbalimbali waliotia nia katika jimbo hilo

Mbali ya usomi wao lakini zaidi ni kumshinda Waziri mstaafu wa siku nyingi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo William Ngeleja

Hamis Tabasamu mwaka 2015 aligombea ubunge wa Sengerema kwa tiketi ya CHADEMA na kushindwa kumg'oa Ngeleja. Mwaka 2017 Tabasamu alihama CHADEMA na kwenda kuunga juhudi za Mheshimiwa John Magufuli kwa kile alichoita amechoshwa na upinzani kupinga kila kitu hasa hatua zilizochukuliwa kwenye makinikia

Wafuatao ndiyo walikuwa watia nia wa Sengerema

1. Hamis Tabasamu- Std 7
2. William Ngereja - Master in Law
3. Philemon Tano - Master in HRM
4. Joshua Shimiyu- Master in HRM
5. Lawrence Masha- Master in Law
6. Yohana Kasenga- Shahada ya elimu.
7. Ndakama Salang’anya- BA Econom
8. Kelvin Natto- BA in Law
9. Tumaini Limbe-Shahada ya Kilimo
na Mifugo
10. Yunge Maige- Bachelor ya Accounts
11. Mlyambelele Levi Ng'weli- Sheria + Post Graduate Diploma in Legal Practice.
12. Veronica K. Mugoyela- shahada ya Uzamivu fani ya Pharmacy.
13.William J.Tega PGD -Economic Diplomacy
14. Eng. Suleman Daudi Arthur Nkalango - Ph.D In Information and Telecommunication Engineering
15. Evarist Clement Matulanya- Shahada ya Ualimu
16.Dotto Joseph Ndemella-Master of Arts in Economics
17.Dr Godwin Silas Macheku,Adv.dipl (SRHR),MD(doctor of medicine),MMED (masters of medicine)(obgyn)
18. Onesmo Yegella Ntoneji, Masters in Procurement and supply chain management. PGD in Air Transport Management, (Airport operations)

Jimbo la Sengerema hawa ndio waliotia nia na namba 1 Ndo kashinda.
 
Sio kuzuiliwa mshahara tu, bali na hatua za kinidhamu zinaweza kufuata.

Ukitia nia unatakiwa uombe likizo bila malipo na utaratibu wa kurejea kazini baada ya kura za maoni kumalizika umeelezwa.

Magufuli huu waraka kaukuta na hakuna alichoongeza wala kupunguza, shida iliyopo ni uelewa kwa baadhi ya watumishi maana ya likizo bila malipo.
 
Hugo mnayempelekea kilio chenu ndio alito maelekezo kuwa mkatwe
 
Serikali imefanya jambo la maana sana,,,,walitakiwa wajitoe utumishi wa umma kabisa,maana washaharibu taswira zao na ofisi wanazotumikia.
 
Kuna kutoa Nia ndani ya chama na Kuna kuteuliwa kugombea ndani ya chama baada ya kutia nia.ukisha teuliwa na time ya uchaguzi ndipo unapoandika barua kujiondoa kazini na kulipwa mafao yako.mwaka huu umekuwa kinyume kabisa kwani kutoa Nia sio lazima uchaguliwe kugombea.mwenye hiyo Sheria aiwekwe hapa tuisome.Hii itachangia Sasa badala ya mtumishi kutoa Nia hadharani watajiunga na upinzani kwa Siri kubwa kukingoa chama tawala madarakani.
 
Weka Sheria hiyo hapa Kama unachokiongea unakifahamu au wewe Ni wale walio unga unga madarasa na vyuo.
 
Tia nia ukiwa umejipanga. Kama unashindwa kusimama baada ya kutolipwa mwezi mmoja tu wa mshahara, je utawezaje kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya jimbo zima?
Wapuuzi hao.Walitaka kuacha kupokea mshahara wenye heshima ili wakapokee posho zitokanazo na makusanyo ya ushuru wa mapera!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Waumishi wa umma wanastahili sana mateso hasa hata na zaidi kwasababu wamekuwa watu wakujipendekeza kila mtu kwa nafasi yake. Ushauri wangu sasa hivi ni wakati wa kuipanga na kuhakikisha wanawashawishi marafiki na wategemezi wao wote wanamuondoa huyu bwana mkubwa madarakani kupitia sanduku la kura maana kwakweli ni janga kwako
 
Mwaka 2000,2005,2010 na 2015 walichukua mishahara ya waliotia Nia? Kule Jimbo la biharamulo na chato wakati huo mgombea alikuwa Nani na alipotia Nia akiwa walimu sengerema sekondari alifanyiwa hayo?
 
Sheria zingine za kipumbavu.

Kutia nia kwenye CHAMA haina uhusiano na kazi yako ya Taifa. Hizo ni kura za maoni bado wala ujapata nafasi ya kuwakilisha chama.

Ndio maana issue kama ya MAKONDA Kuachia nafasi ya mkuu wa mkoa kisa katia nia kwenye chama kugombea ubunge ni ujinga.

Rais katia nia kugombea tena mbona ajaachia nafasi yake ya Urais kwa mtu mwingine mpaka Uchaguzi ufanyike?

Nani ameshika nafasi ya Dr. Mwinyi?

Huu ni uchaguzi mkuu serikali mpya ikija itachagua viongozi wake wapya; sio kufuja pesa kuweka watu wapya wakati kuna miezi michahe imebaki serikali imalize mda wake.

Na ndio maana hao wote ni dhulma tu.
 

Ccm Oyeee,wana Ccm tumefurahishwa sana na uamuzi wa serikali.

Mapinduzi daima,daima mapinduzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…