Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Waraka niliokutajia umeusoma? Ni wa mwaka 2015
 
Kuna kada mtumishi jirani yangu naona jana getini kwake alikua amelewa amechafukwa akachoma moto shati lake la chama.

Kila kunguru ana siku yake.
 
Jibu swali,mbona unaleta ngonjera JF
Sio ngonjera mkuu, najua umebanwa mahali panapouma ndio maana unapiga kelele hadi nyumba ya tatu wanasikia. Acha tamaa, ukiamua kwenda kwenye siasa nenda kwa miguu yote, sio sitaki nataka
 
Maisha lazima kukabiliana na lolote,alivyo enda kutia nia ni wazi alizijua hizo changamoto.
 
mkome kujipendekeza kama mashori, siku moja mtakuja kuolewa shauri zenu, sisi tunawachora tu!
 
Mbinu za tabaka tawala kuendelea kutawala..kuweni wapole watawaliwa a.k.a wanyonge..Siasa konekisheni na pesa tofauti na hapo wajumbe lazima wa wale vichwa tu..

#MaendeleoHayanaChama.
 
Kama nawaona mtakavyokuwa mnatembea huku machozi yanawalengalenga tu.Mkiulizwa nini mbaya,mtajibu mnasumbuliwa na miwasho ya macho(😢😢😢😭😭😭😓😓😓)😝😝😝😝😝😝
 
Maisha lazima kukabiliana na lolote,alivyo enda kutia nia ni wazi alizijua hizo changamoto.
Taratibu ziko wazi kabisa, nashangaa huyu mtu kuja kulalamika kwenye mitandao baada ya kuona taratibu zinataka kutekelezwa.
 
Sheria inasema ni marufuku mtumishi wa umma kujihusisha na siasa! Wewe ulikua hujui?
 
Ulipaswa kuzijua standing orders za watumishi wa umma kabla ya kuamua kwenda kutia nia ya kuwania kazi za kisiasa. Standing orders zinasema wazi kuwa watapewa likizo ya bila malipo kwenda kutia nia. Wakishindwa kuchaguliwa kugombea huo ubunge au wakimaliza vipindi vyao vya ubunge wataomba kurudi kazini. Muda ambao hawakuwa kwenye civil service hautahesabika hata kwenye kukokotoa pensheni zao watakapostaafu. Huko nyuma (1990s) walikuwa hawaruhusiwi kabisa kuwania kazi hizo za kisiasa. Iliwabidi waache kazi kama wanataka na kupoteza kabisa pensheni zao. Kuna wakati walikuwa hawaruhusiwi hata kuwa wanachama wa chama cho chote cha siasa kama ilivyo hadi sasa kwa millitary servants.

NB. Ukishatia nia ya kuwania uongozi wa kisiasa unatia doa kwenye utumishi wako kama civil servant.
 
sheria mbona iko wazi hapa ofisini kuna mshikaji ni dereva naye alichukua fomu ya ubunge nikajisemea kimoyomoyo hiyo ela si bora angempa mke wake apeleke kwenye kikoba
 
Kabla ya kulalamika kasome kwanza kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2017, na waraka uliotolewa kuelekea uchaguzi mkuu na katibu mkuu utumishi Dr Rauriani Ndumbaro,waraka huo uliweka wazi kila kitu kuhusu watumishi wa umma wanaotaka kugombea, changamoto ninayoiona watanzania wengi ni wavivu wa kusoma.

Iko hivi endapo mtumishi wa umma akichukuwa fomu ya kuomba uteuzi katika chama chochote cha siasa anatakiwa kuomba likizo isiyokuwa na malipo kwa kipindi cha mwezi mmoja ili apate nafasi ya kutosha ya kufanya kampeni hii itaepusha mtumishi kufanya kazi chini ya kiwango sote tunajua mziki wa kampeni ulivyo.

Na endapo utapata uteuzi kukiwakilisha chama katika uchaguzi mkuu utumishi inakoma automatic.

Tatizo wengi mlienda kugombea kwa malengo kwamba hata mkikosa nafasi mlizoomba mnaweza kupata nafasi za uteuzi jambo ambalo siyo kweli kama una sifa na Mungu amepanga unaweza kuteuliwa bila hata kutia nia.
 
Mbona mimi pamoja na kutia nia nimelipwa mshahara au nilisahaulika?
 
Yap,
Mbona mimi pamoja na kutia nia nimelipwa mshahara au nilisahaulika?
Wengi waliotia Nia viti maalum ubunge ccm wameachwa bila kukatwa mishahara. Uko sawa kabisa mfano mkoa wa manyara wote walio Tia Nia wamepewa mishahara yao yote. Hii imeadhibu wengi wa mkoa wa Arusha , Kilimanjaro na dar
 
Lakini sheria hii ilitungwa kwa maudhui yepi?
Kwa faida ya nani?
Nafasi nyeti kabisa kwa mustakabari wa taifa mnaziwekea mazonge zonge kibao kisa nini?
Binafsi naona ipo shida hapa na watunga sheria huenda waliliweka hili kwa maslahi yao. Hawataki kusumbuliwa na wasomi walioko kwenye ajira serikalini
Naomba niungwe mkono sheria hii irekebishwe
Mh Mkuchika tusaidie watumishi wako kwenye hili hakika nakwambia utaacha alama kubwa sana kwa wafanyakazi kama utaamua kufanya mabadiliko kwenye sheria kandamizi hii
ASANTE
 
Tumeona sheria hii imetumika kwa waliotia nia ubunge wa majimbo tu kupitia CCM Ila Sheria hii imewakwepa walio tia Nia ubunge ccm kupitia viti maalum .chama hicho hicho na nchi moja.
 
Tumeona sheria hii imetumika kwa waliotia nia ubunge wa majimbo tu kupitia CCM Ila Sheria hii imewakwepa walio tia Nia ubunge ccm kupitia viti maalum .chama hicho hicho na nchi moja.
Nilisikia kuna watia nia furani waliohatarisha nafasi za wenye chama chao ndo wamelengwa zaidi. Sijui kama kuna ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…