Poleni sana wadau wenzangu kwa kadhia iliyotukuta pamoja. Tunaamini tulitumia haki yetu ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa. Tatizo ni kuwa kwenye taasisi za serikali. Nawapa pongezi wenzetu wa taasisi na mashirika yasiyo ya serikali kwa kutumia haki yao bila bughudha. Tuzidi kushikamana kipindi hiki cha majonzi mara tatu. Kwa kuambulia kura 0,1, na 3, kwa kufiwa na kipenzi chetu Mkapa, na kwa kuanza maisha mapya ya kuomba omba nauli na kukopa kwenye maduka ya mpemba na mangi. Tusijali, Mungu atatufuta machozi yetu.