Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Katika hili sioni tatizo la Serikali,

Unaenda kwenye issue ya kisiasa ambayo itakuchukua si Chini ya miezi miwili halafu unataka ulipwe mshahara bila kufanya kazi kwa kipindi chote hicho...!

Imagine wewe ndo kiongozi wa taasisi fulani yenye watumishi 200 halafu 100 wote wameondoka kwenda kugombea, huoni kuwa kwa kipindi taasisi lazima ipalalyse kwa kipindi hicho chote....! Hautaweza kuajiri sababu vote yako imeshiba watumishi ambao unawalipa mshahara wa bure.

Huo mwongozo uko pale kuhakikisha utoaji wa huduma za Umma hauathiriwi na wimbi la utia nia na ndio maana kuna nafasi zinalazika kuzibwa eidha kwa kuajiri au kuteua na ikishajazwa uliyeenda likizo ndo basi tena.

Muhimu ni watumishi kuelewa sheria, kanuni na miongozo ili kuepuka kusombwa tu na pepo za kisulisuli.
 
Mawaziri nao hii inawahusu ama wale wa local gvt tu?
 
W
Wengi wao machakato haujawachukua hata majuma wawili - inakuwaje wakatwe mshahara wa mwezi mzima? Hovyo kabisa!
 
Endeleni na huo waraka namba1,Ila kwa Hali halisi ya kimaisha, watumishi hawana Raha ,na Kuna uwezekano watumishi kutimukia upinzani kwa Siri kubwa.watumishi wa umma wanateseka Sana,mishahara tangu 2015 Hadi leo uko pale pale, hata nguo za kuvaa watumishi wavae waende kazini wameshindwa kununua, watumishi wanakula mlo mmoja.
 

Wa kutimka watatimka tuu. Ila sheria zifuatwe kazi iwe kazi na siasa ibaki kuwa siasa
 
Kwa hiyo alipwe mshahara bila Kufanya kazi?
 
Tumeona sheria hii imetumika kwa waliotia nia ubunge wa majimbo tu kupitia CCM Ila Sheria hii imewakwepa walio tia Nia ubunge ccm kupitia viti maalum .chama hicho hicho na nchi moja.
Nasikia wana mpango wa kutufukuza kazi kwa tusioomba ruhusa.
 
Nimedokezwa kuwa uko mpango wa kutufukuza kabisa kazi kwa wote tusioomba ruhusa. Taarifa zinachanganya sana. Kwa kweli ccm yetu imetukomesha.
 
Nimedokezwa kuwa uko mpango wa kutufukuza kabisa kazi kwa wote tusioomba ruhusa. Taarifa zinachanganya sana. Kwa kweli ccm yetu imetukomesha.
Sheria ilitaka uombe ruhusa.
 
Maelekezo mengine yametolewa leo.Hakutakuwa na adhabu kwa watia nia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…