Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Sasa mwezi wa saba wote hamjafanya kazi yoyote zaidi ya kupiga sarakasi za uteuzi.Mnataka mshahara wa nini?
 
Huyu Neema Musomba wa kwa TR huwa mnoko kweli kweli!
 
Kichwa Cha habari kinajieleza.
Mh Rais wa Tanzania tunaomba upokee na ukisikie kilio Cha watumishi wako zaidi ya watumishi 1,000 wameshitishiwa mishahara yao ya mwezi July,2020.

Watumishi hao wakati wanaomba kutia Nia nafasi mbali mbali hawajajulishwa kuwa kutia Nia utakatwa mishahara ya July 2020. Cha kusikitisha zaidi watumishi hao walinunua fomu ya kugombea kwa TSH 100,000 na kuchangia gharama za uchaguzi ili fedha hizo zitumike kuwalipa wajumbe kila mgombea amechangia CCM kuanzia TSH 400,000 Hadi 1,000,000 .

Mwisho watumishi wameishia kukosa kura za maoni na kukosa mishahara yao ya mwezi July 2020. Baadhi ya waliokatwa mishahara walikuwa kazi kwao muda wote Ila wamekatwa mishahara yote bila kujali na bila kuwa na kiambatisho chochote .Cha kushangaza zaidi watumishi hawajui hatima yao ya mishahara ya mwezi August 2020 itakuwaje.

Watumishi kwa umaskini wao wamekichangia chama tawala fedha za uchaguzi kinyume chake serikali inayoongozwa na chama tawala imekuja kusitisha mishahara ya hao watumishi walio maskini na hawana kipato kingine .Sasa hawajui wale wapi,Kodi za nyumba wapate wapi, umeme na maji walipeje,Ada za watoto watoe wapi,hawajui wakope wapi, na bado mkumbuke pia ni wapiga kuwa wa CCM .tunaomba kilio hiki Cha wafanyakazi kisikilizwe Hali ni mbaya mbaya mbaya sanakwa watumishi wa Umma hata nauli za kwenda makazini mwezi huu wa nane hawana.
 
Wamechangia chama sio serikali. Halafu hao watumishi wasiojua kuwa ukitaka kwenda kugombea mchakato wa kura za maoni ili upitishwe kuwa mgombea ni lazima uombe likizo bila malipo ni wajinga hata hiyo nafasi ya utumishi wa umma hawakustahili. Utaratibu upo wazi tangu muda mrefu, sio utaratibu mpya wala si jambo jipya.
 
Mshika mawili moja humponyoka, tatizo lenu mnashupaza shingo zenu.
 
Vyama zilivyosajiliwa ni zaidi ya 18. Kwa nini mlikichangia chama kimoja tu? mnastahili adhabu hiyo.
Watumishi kwa umaskini wao wamekichangia chama tawala fedha za uchaguzi kinyume chake serikali inayoongozwa na chama tawala imekuja kusitisha mishahara ya hao watumishi walio maskini na hawana kipato kingine .
 
Mnasitahili kuachishwa kazi kabisa ili vijana wetu walioko mtaani wapate ajira pia.
 
Sasa Rais anahusikaje hapo?

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…