Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Watumishi wa Umma waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa kukatwa mshahara wa mwezi Julai

Kuna tangazo linazunguka juu ya kutolipwa mishahara kwa wafanyakazi wa umma ambao walichukua fomu za kuomba kupata ridhaa kutokak chama cha mapinduzi ili wapeperushe bendera ya kuwania nafasi za ubunge.

Binafsi naunga mkono katazo la kutolipwa mshahara wa mwezi huu wa julai, ila kwa mtazamo wangu hawa wangefukuzwa na kufutwa kabisa katika utumishi wa umma.

Hawafai na walafi. Nchi imejaa vijana wengi waliohitimu vyuo wakihaha kutafuta kazi. Jitu limepewa kazi linatamaa ya kutaka Ubunge, hawa hawafai kbs ni bora wafukuzwe kazi wakalime. Ni ujinga wa hali ya juu kucheza na kazi.

Mheshimiwa Rais ebu fanya kitu hapa. Hili la kuwapumzisha wateule wako liende mbali zaidi ama itungwe sheria kali ya kuwabana hawa wenye tamaa.
 
.hii sio order kutoka juu kwel kwamba watumishi wana tamaa hawaridhiki na wanachokipata ?
IMG-20200721-WA0000.jpg
 
Yaani mtu umeenda kugombea, umeomba ruhusa ya siku 3, kufika jimboni unaambiwa chama hakina fedha za kusafirisha wapiga kura, umechangia mshahara wako laki 9, ili wapiga kura wale, wanywe, halafu unapata kura moja , tena huku unasikia mshahara wa julai hamna. CCM Mungu anawaona.

Kwa kiasi kikubwa uchaguzi huu umesaidiwa na watumishi
 
YALE YALE YA WAFANYAKAZI HEWA

HIVI KWA NINI TUSIRUDISHE AZIMIO LA ARUSHA 😎
 
Kama wateule wa Rais kabisa waliotia nia ya kugombea ubunge wamefutwa kwenye nyazifa zao na kuteuliwa wapya, watumishi wa umma walioacha ajira zao wakaenda kugombea ubunge wao ni nani mpaka waachwe kwenye kazi zao waendelee kupokea mshahara walioona hauwafai wakaenda kutafuta mshahara wa wabunge?.
 
Back
Top Bottom